MKURUGENZI
wa Jiji la Tanga Sipora Liana akizungumza wa maadhimisho ya siku ya
mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya kwenye viwanja vya Urithi Jijini
Tanga
Meneja
Mradi wa EELAY wa Shirika la Brac Tanzania Hope Jasson akizungumza
wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya
kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga ambapo alielezea namna Shirika
hilo lilovyowezesha zaidi wasichana 900 kupata fursa ya kumaliza elimu
ya sekondari kupitia mpango wa muda mfupi chini ya taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima
Diwani wa Viti Maalumu (CCM) akizungumza wakati wa maadhimisho hayo |
Na Oscar Assenga,TANGA.
SHIRIKA la Brac Maendeleo Tanzania limewawezesha zaidi ya Wasichana 900 walio na umri kati ya miaka 15-24 kupata fursa ya kumaliza elimu ya Sekondari kupitia mpango wa muda mfupi chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Hayo yalibainishwa leo na Meneja Mradi wa EELAY wa Shirika la Brac Tanzania Hope Jasson wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.
Alisema Shirika hilo kwa msaada wa kifedha kutoka NORAD (Norwegian Agency For Development Cooperation) inatekeleza mradi wa miaka minne unaoitwa (Education Empowerment and Life Skills For Adolescent na Young Children –EELAY).
Mradi huo unatoa elimu ya Elimu,Uwezeshaji na Stadi za Maisha katika Halmashauri ya Jiji la Tanga na wilaya ya Korogwe tokea mwezi June mwaka 2018 hadi Desemba 2022 ambapo mpango huo ulikuwa ni wa muda mfupi yenye matokeo chanya (ALP) kuwasaidia katika kukamilisha miaka minne ndani ya miaka miwili .
Akieleza mafanikio makubwa ya mradi huku akieleza kwa sasa wanaendelea kutoa huduma kwenye vituo 30 vya masomo chini ya usimamizi wa Jamii,kati ya hivyo 20 viko Halmashauri ya Jiji la Tanga na 10 katika wilaya ya Korogwe.
“Lakini asilimia 86.8 ya wasichana walioko kwenye rika balehe wamefaulu na kupewa cheti cha Elimu ya Sekondari tangu 2017 hadi 2021 kati yao 51 wamejiunga na masomo ngazi za juu katika shule za Serikali na shule binafsi,wanafunzi 10 kutoka kundi la mwaka 2016 walijuunga na vyuo vikuu katika kozi za shahada ya kwanza”Alisema
Alisema takribani watoto 1670 kati ya umri wa miaka 3-5 walipata elimu ya makuzi,malezi na maendeleo ya awali ,madarasa mapya 22 yamejengwa na madarasa 13 yamekarabatiwa katika shule za Serikali na kutumia kama vituo vya kusomea vya watoto vijana.
“Walimu 41 wa elimu ya awali kutoka shule za Serikali walipatiwa mafunzo juu ya mtaala wa elimu ya awali na kutoa msaada wa rasilimali kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya kufundishia”Alisema
“Lakini pia ni matumaini yetu kama Shirika baada ya Desemba 2022 Halmashauri ya Jiji la Tanga itaendelea na kazi ya Usimamizi na uangalizi huku jamii husika ziliendelea kutekeleza mradi hivyo mafanikio yataendelea kuonekana”Alisema
Awali akizungumza katika Maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Sipora Liana alisema wakati wanaadhimisho siku ya mtoto wa Afrika ni vema kuimarisha ulinzi wa mtoto ili kuepusha ukatili dhidi yake na kutafakari kupata nafasi ya kuelimisha jamii juu kujenga taifa lenye uwasa na kutokokemeza matukio ya ukatili wa kijisia na ukatili dhidi yao
“Mkiona mnafanyiwa vitendo vya ukatili toeni ripoti waambieni walimu,mama,baba njoo pia kwangu mje mniembie lengo ni kufikia maendeleo endelevu kuongeza ushiriki wa watoto wa kike kwenye uongozi na kubadiliusha uzoefu kwenye masuala kichumi,kijamii na kiutamaduni”Alisema
Alisema zipo changamoto ambalimbali ambazo zinawakabili watoto na kusababisha kuzorotesha maendeleo yao ikiwemo ukatili huku akitoa wito kwao kuache kwenda mahali ambapo ni hatarishi.
“Bado Jamii na watoto wanajukumu la kufanya kuimarisha ulinzi hususani mtoto endapo matukio ya ukatili au dalili za kufanyiwa ukatili zinapotokea ili kuweza kuepukana na kadhia hizo”Alisema
“Naomba niwatie shime watoto wa kike ni kitovu cha maendeleo na wana wajibu wa kushiriki katika shughuli zote za maendeleo na kusoma kwa bidii pia mzitambue haki zenu ili kupunguza matukio ya ukatili wa kijisnia dhidi yenu”Alisema
Hata hivyo alisema pamoja na changamoto wanazopitia watoto Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu bado
Naye kwa upande wake akisoma risala ya siku hiyo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkwakwani Sumaiya Ally alisema katika siku ya mtoto wa Afrika wanatoa ombi kwa familia,Jamii na Serikali kwa ujumla kuungana kwa pamoja katika kuhakikisha ulinzi kwa mtoto unaimarishwa na matendo ya ukatili yanatokomezwa ili kujenga kizazi kilicho bora.
“Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunatekeleza haki za mtoto zinazoanishwa kwenye sera ya mtoto ya mwaka 2008 ambazo ni haki ya kuishi, kuendelezwa,kushiriki,kulindwa na kutokubaguliwa”Alisema Sumaiya
Hata hivyo alitoa ombi kwa Serikali ,Mashirika yasiyoya kiserikali pamoja na wakazi wa Jiji la Tanga kutambua na kutafuta ufumbuzi wa matatizo wanayoyapata watoto wenzao wenye ulemavu,yatima na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
“Kwani watoto hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika maisha kwa mfano unyanyasaji ,kokosa malezi mazuri kutoka kwa wazazi na walezi na hivyo kukosa haki zao za Msingi “Alisema