Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akitazama moja ya kifaa malumu cha kujifunzia utengenezaji wa ndege kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es SalaamNaibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akwa kwenye chumba maalumu cha kujifunzia uendeshaji wa ndege kwa vitendo kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es SalaamNaibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akipata picha ya pamoja na wadau wa elimu kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akitazama moja ya kifaa cha ndege ambacho kipo kwaajili ya kujifunzi utengenezaji wa ndege kwa vitendo kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es Salaam.Pembeni yake ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Zacharia MganilwaNaibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa uhandisi wa matengenezo ya ndege kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akikata utepe kuzindua chumba maalumu cha kufanyia majaribio kwa vitendo kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, akizungumza leo Juni 17,2022 kwenye hafla ya uzinduzi wa vifaa vya uhandisi wa matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Jijini Dar es Salaam
************************
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezundua vifaa vitatu vya uhandisi wa matengenezo ya ndege vinavyo ghalimu zaidi ya Sh. Bilioni 2 katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kuzalisha wataalamu wenye weledi mkubwa.
Vifaa hivyo, vimezinduliwa jana chuoni hapo na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, alisema kupitia mradi wa kukuza ujuzi ambao upo kwenye nchi kama tatu za Afika Mashariki wameweza kupata fedha kutoka benki ya dunia na kununua vifaa hivyo.
Amesema vifaa hivyo vitatumika vizuri kuwapa ujuzi wenye weledi mainjinia wanaohusika kutengeneza ndege, ambapo wataweza kufanya kazi za mikono, kwa sababu anapofundishwa lazima ashike chombo.
Prof. Nombo, amesema injinia anapotoka katika chuo hicho akienda kwenye karakana ya ndege moja kwa moja anaweza kufanya matengenezo yanayotakiwa kwa sababu alipokuwa kwenye mafunzo alitumia vifaa.
“Kama mnavyojua nchi yetu ina ndege nyingi na itaendelea kuongeza nyingine, kwa hiyo tunahitaji kuwa na injinia wenye uwezo wa kuhudumia ndege kwenye matengenezo na kutoa huduma zenye ubora,”alisema Prof. Nombo
Pia, Naibu huyo alitoa wito kwa wakufunzi kutumia vifaa hivyo kwa lengo tarajiwa na pia anaamini watawapa wanafunzi maelekezo mazuri na halisi katika kutumia vifaa hivyo na kuwataka wanafunzi kutunza vifaa hivyo ili viweze kudumu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Zacharia Mganilwa alivitaja vifaa hivyo kuwa ni kompyuta za kisasa ambazo zinatumika kufundishia wahandisi wa ndege duniani.
Amesema vifaa vingine ni VMT ambavyo vinatumika Marekani na Air bus ya nchini Ufaransa, ambapo wahandisi wao wanatumia vifaa hivyo, inaonesha jinsi gani NIT ipo kimataifa zaidi katika kupata watalaamu wenye weledi.
“Amezindua injini mbili za ndege ndogo zinazotumiwa na Tanapa, uwanja wa ndege Terminal one na kule Arusha na Zanzibar hizo ndege zinatumia piston injini na zinatumia mafuta kama ya taa,”. Amesema Prof.Mganilwa