Afisa Raslimali wa Barrick Bulyanhulu, Renatus Malawa, akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine kilichopo Mwanza kuhusu kuchangamkia fursa za kujikwamua kiuchumi wakati wa Kongamano la kuwajengea uwezo lililotayarishwa na taasisi ya AISEC na kudhaminiwa na Barrick lililofanyika chuoni hapo
Afisa Raslimali Mwandamizi wa Barrick North Mara, Daniel Paul akiwagawia zawadi ya Flash Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine kilichopo Mwanza wakati wa Kongamano la kuwajengea uwezo lililotayarishwa na taasisi ya AISEC na kudhaminiwa na Barrick, lililofanyika chuoni hapo.
Mkurugenzi Rasilimali watu wa Taasisi ya kuwaendeleza vijana kitaaluma baada ya kuhitimu (AIESEC) Richard Balayazi, akiongea wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Augustine Mwanza, wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la kuwajengea uwezo lililotayarishwa na taasisi ya AIESEC na kudhaminiwa na Barrick, lililofanyika chuoni hapo.
Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Augustine Mwanza, wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la kuwajengea uwezo lililotayarishwa na taasisi ya AIESEC na kudhaminiwa na Barrick, lililofanyika chuoni hapo.
Baadhi ya Wanafunzi wa SAUT wakiwa katika picha ya pamoja na watoa mada wakati wa kongamano hilo.
**
Kongamano la kuwajengea wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kwa ajili ya kuweza kumudu kuingia katika soko la ajira, kujiajiri sambamba na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kudhaminiwa na kampuni ya madini ya Barrick kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limefanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, kilichopo jijini Mwanza.