Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Serikali katika Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Dodoma.
…………………………..
Na AlexSonna_,DODOMA
TANZANIA imeendelea kuandika historia katika maendeleo ya sekta ya utalii hasa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kurekodi filamu ya Royal Tour iloyozinduliwa hivi karibu.
Hayo yamesemwa jijini na msemaji wa mkuu wa serikali Gerson Msigwa, wakati akizungumza na waandishi wa hahari amesema kuwa matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia yameanza kuonekana kwani idadi ya watalii imeanza kuongezeka kwa kasi kubwa katika maeneo ya vivutio vya utalii na katika mahoteli.
“Takwimu kutoka Hifadhi za Taifa (TANAPA) zinaonesha Aprili na Mei 2022 idadi ya watalii waliotembelea maeneo yetu ya hifadhi 22 yanayojumuisha Serengeti, Manyara, Mikumi, Nyerere, Udzungwa, Ruaha imeongezeka hadi kufikia watalii 115,198 ambapo kati yao watalii wa ndani 71,593 na watalii wa nje 43,605 ikilinganishwa na watalii 59,664 ambapo watalii wa ndani 46,624 na watalii wa nje 13,040 wa Aprili na Mei mwaka jana,”alisema
Msigwa alisema “Ongezeko hili pia limeongeza mapato kutoka Sh.bilioni 5.7 hadi kufikia Sh.bilioni 15.559.
Aidha, alisema katika Hifadhi ya Eneo Maalum la Ngorongoro takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha Aprili na Mei 2022 idadi ya watalii imeongeza hadi kufikia 51,044 ambapo wa ndani ni 25,150 na watalii wa nje 25,894 ikilinganishwa na watalii 22,954 wa Aprili na Mei mwaka 2021.
Alisema mapato kutoka Ngorongoro kwa kipindi hicho yameongezeka kutoka Sh.bilioni 2.585 hadi kufikia sh.bilioni 10 ambapo ni ongezeko la asilimia 289.
Msigwa amsema kuwa lengo la serikali ni kufikisha watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo 2025.
Hata hivyo Msigwa aliwataka Watanzania kushiriki zoezi la sensa linalotarajia kufanyika Agost 23 mwaka huu nchini.
“Sensa ya mwaka huu ni ya kidijitali zaidi lazima kila mmoja wetu ashiriki ili tuwe na sensa bora ambayo mataifa mengine yatakuja kujifunza”alisema
Amesema kuwa maandalizi ya sensa yamefikia asilimia 88 na ugawaji wa maeneo ya kuhasabia watu kwa Zanzibar na Tanzania Bara yamefikia asilimia 100 kinachoendelea hivi sasa ni utoaji wa elimu kwa wananchi.