Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mwenye shati
la Draft Bw. Raymond Mndolwa akizungumza na wataalam alipokuwa kwenye banio la skimu ya kilimo cha
umwagiliaji Dakawa Wilayani Mvomero.
Mkuu
wa Wilaya Mvomero Mhe. Halima Okashi akizungumza wakati wa kikao cha
wataalam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa yaUmwagiliaji, ambao hawapo
pichani Ofisini kwake mapema leo
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw.
Raymond Mndolwa akifuatilia mazungumzo ya Kikao cha wataalam na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,
mapema leo
Na; Mwandishiwetu–Mvomero
Mkurugenzi wa Tume ya Taifaya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mndolwa, amesema hatasita kusitisha mkataba wa mkandarasi yeyote
yule atakayekosa vigezo vinavyotakiwa hatakama atakuwa ameanza kazi ya ujenzi ama ukarabati wa miundombinu ya kilimo
cha umwagiliaji.
Bw.Mndolwa amesema hayo mapema leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro
,baada ya ziara ya ukaguzi maalum wa skimu ya kilimo cha umwagiliaji Msufini,
ambapo yalijitokeza makosa ya kitaalam kabla ya ukarabati wa skimu hiyo yaliyopelelekea miundombinu ya skimu hiyo kutofaa.
“Niliamua
kuitembelea skimu ya Msufini,wilayani Mvomero kwasababu ilikuwa na
matatizo,ni skimu ambayo tayari alikuwa amepewa mkandarasi kwa ajili ya
kuiendeleza lakini maandalizi ya skimu ile hayakuwa mazuri kiasi
cha kupelekea wataalam kuruhusu mkandarasi kwenda site wakati hakukuwa na site ambayo inaweza kutekeleza kaz ihiyo.”
Alisisitiza Mndolwa
Aliendelea kufafanua kuwa mapungufu haya yapo ndani ya Ofisi yake,
“Nimewaambia hakuna mradi ambao tutaufanya bila kuwa na uhakika na chanzo cha maji.
Skimu hiyo imefanyiwa kazi wakati chanzo cha maji tayari kilikuwa kimekwisha athirika.”
Alibainisha Mkurugenzi Mndolwa
Aidha Bw. Mndolwa ametoa maelekezo kwamba Mradi wa kilimo cha
Umwagiliaji Msufini hauwezi kutekeleze ka hivyo wataalam warudi wakaanze kujipanga upya kufanya tafiti.
Akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Bw. Mndolwa aliomba ushirikiano na Uongozi wa Wilaya hiyo katika suala zima
la elimu kwa umma kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji kwamba jambo hilo lipewe kipaumbele.
Na
kushauri kuwe na ushirikiano na wadau kama
vile, TANROADS ambao walitengeneza barabara inayoelekea Turiani yenye
Daraja ambalo limesetiwa na kuhamisha mto Mvomero kiasi kwamba kwa
baadae inaweza kuleta athari kwenye makazi yawatu.
Mkurugenzi Mndolwa alibainisha kwamba,
“Wengine wote wahakikishe kama wanasema wanafanya miradi yoyote wawe na taarifa zote,
uzembe kama uliotokea Msufini niuzembe wawataalam ndani ya Tumeya Taifa ya Umwagiliaji,
hakuna vinginevyo na wao watawajibika kwa namna yao na mimi sitakubali uzembe kama huo uliotokea ujirudie tena.”
Mndolwa
aliendelea kusema kwamba, hatutafanya mradi ambao hakuna wataalam,
“kwa hiyo tutahakikisha kwanza wataalam wanapita tutahakikisha tuna
washirikishana
wale wengine(wadau), kama watu wa Bonde,watu wa mazingira na kuhakikisha
kwamba,mradi unaotakiwa kujengwa unakuwa endelevu,
kwa hiyo hatakama tunataka kujenga bwawa lazima tufikirie,hili bwawa au
skimu je
miundombinu hii itakuwa endelevu kwa muda gani, kwa hiyo kitu muhimu
nitachotaka kusema nikwamba utaalam nitautumia kwenye kazi yangu
kuhakikisha kwamba unatupa majibu sahihi.”Alisisitiza
Awali,
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bi Halima Okashi,
alisema kuwa kumekuwa nau kakasi katika ukarabatiwa Skimu ya kilimo cha
Umwagiliaji Msufini,
na changamoto ni kubwa katika skimu nyingi wilayani Mvomero na fedha
nyingi za Serikali zimetumika na kushauri kuwepo kwa ushirikishwaji
mkamilifu wa wadau katika kazi hizo.