Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania(TALIRI) kwenye ofisi za Kanda inajumuisha mikoa ya Dar,Pwani Morogoro na Tanga Dkt. Zabron Nziku wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za sayansi na teknolojia yanayofanyika mjini Tanga.
Afisa Utafiti Mkuu kiongozi kutoka Tume ya Sayansi na teknolojia Dkt Bakari Msangi akitoa mada kwenye mafanzo hayo kuhusu umuhimu wa utafiti nchini Tanzania pamoja na umuhimu wa kusambaza matokeo ya utafiti.
Afisa Utafiti Mkuu kiongozi kutoka Tume ya Sayansi na teknolojia Dkt Bakari Msangi akitoa mada kwenye mafanzo hayo kuhusu umuhimu wa utafiti nchini Tanzania pamoja na umuhimu wa kusambaza matokeo ya utafiti.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania Mkoani Tanga Amina Omari akieleza namna mafunzo hayo yatakayoweza kuwasaidia |
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo hayo
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo hayo
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo katikati ni Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoa wa Tanga Pascal Mbunga
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kushirikiana na taasisi zinazojuhusisha na tafiti mbalimbali ili waweze kupata taarifa sahihi kwa kutumia takwimu ili kuweza kuwahabirisha watumiaji wa mwisho.
Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa Mifugo Tanzania kwenye ofisi za Kanda inajumuisha mikoa ya Dar,Pwani Morogoro na Tanga Dkt Zabron Nziku wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za sayansi na teknolojia yanayofanyika mjini Tanga.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SIDA) yanayoendelea kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga.
Dkt Zabron ambaye pia ni Mtaifiti wa mambo Mifugo lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuona namna waandishi wa habari kuwajengea uwezo kuweza kushirikiana kati yao na watafiti huku wakitegemea watu kwa kutumia teknolojia sahihi zilizotokana na tafiti wanaweza kupiga hatua kubwa na nchi kupata maendeleo.
“Kwa sababu Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa viwanda hauwezi kuja bila kuwepo tafiti mbalimbali kwenye Nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo,mifigo,ardhi na maeneo mengine hivyo niipongeze Costec kwa kuja na mpango huo “Alisema
Alieleza kwani waandishi wa habari wamekuwa ni kiungo muhimu kati ya watu na wadau mbalimbali kuweza kupata taarifa sahihi za kuripoti kuhusiana na mambo ya utafiti.
“Lakini pia nitoe wito kwa waandishi wa mikoa ambayo imeshiriki mafunzo hayo wayatumie kwa umakini waelewe kwa namna gani wanaweza kuwa na uwezo wa kuripoti taarifa sahihi zinazotokana na mambo ya utafiti”Alisema
Alisema kwamba watafiti wakitafiti na kupata matokeo mbalimbali yanaweza kuwa hayana tija kwa sababu yanatumia fedha kama hawajaweza kuwafikia walengwa na wadau mbalimbali wa hizo tafiti.
“Kwa mfano kwenye eneo ambalo ninafanyia kazi tukiweza kutafiti namna bora au mifugo bora inayoweza kutoa maziwa kwenye ukanda wa pwani huyo mnyama watabaki naye na taarifa zitabaki kituoni lakini kwa kuwatumia waandishi wa habari wanaweza kuzichukua taarifa sahihi zilizofanyiwa utafiti kuweza kuubarisha umma wa watanzania hivyo wanaweza kupata teknolojia sahii inayohusiana na mifugo”Alisema
Alisema namna pekee yake ya kutoa maamuzi ambayo yanatija ni baada ya kuwa na taarifa za kitafiti ambazo zina ushahidi ili zitakuongoza kwenye kufanya maamuzi na kuyatumia kwenye kuendeleza Taifa.
Dkt Bakari alisema utafiti ni shughuli ambayo ina mambo mengi ya uwekezaji kwa sababu unatumia fedha nyingi kuwasomesha watafiti na kuandaa maeneo ya utafiti na kufanya utafiti kwa kutumia gharama hivyo ni muhimu kuhakikisha kila ulichokipata kinatumika kuendelea ,kuongeza uzalishaji na tija kwa Taifa.
Mafunzo hayo yanajumuisha waandisi kutoka mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Morogoro na Pwani