Ni katika ziara ya RAISI wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa
Hayo yamebainishwa tarehe 8 juni 2022, katika Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamuro, Mkoani Kagera.
“ Mhe Rais ulituagiza Ofisi ya Rais -TAMISEMI kuwa hutaki kuona majengo ya hospitali yanabaki kuwa maboma, lakini pia ulituelekeza ujenzi wa Hospitali hizi, Vituo vya Afya na Zahanati lazima ukamilike ili wananchi wapate huduma, nikuhakikishie Mhe. Rais ujenzi wa miundombinu hii itakamilika kwa wakati na ubora zaidi” Bashungwa
Aidha, Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwekeza fedha kwaajili ya uboreshwaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya msingi, barabara pamoja na miundombinu ya elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamiro, Bashungwa amesema miundombinu hii inakwenda kuboresha maisha ya wananchi wa Biharamuro na Mkoa wa Kagera kwa ujumla.
Kwa upande mwingine, Bashungwa amesema kutokana na maelekezo aliyotoa Mheshimiwa Rais kuhusiana na zao la Kahawa ambalo kwa asilimia kubwa linalozalishwa Mkoani Kagera maelekezo hayo yameleta matumani makubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo kwakuwa bei ya kahawa imepanda hadi kufikia shilingi 3720 kwa kilo.
“Muelekeo uliotoa Mhe, Rais katika zao la Kahawa , matumaini ni makubwa Mwaka jana ulifanyika mnada wa zao la Kahawa aina ya Radika limeuzwa kwa bei ya 3720 haijapata kutokea” Bashungwa