WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na Makao Makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya kilichofanyika leo Juni 8,2022 Jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na Makao Makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya kilichofanyika leo Juni 8,2022 Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji Prof James Mdoe ,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na Makao Makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya kilichofanyika leo Juni 8,2022 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uthibiti ubora wa Shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bibi Euphrasia Buchumu ,akielezea mafaniko waliyoyapata wakati wa kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na Makao Makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya kilichofanyika leo Juni 8,2022 Jijini Dodoma.
KAMISHNA wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na Makao Makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya kilichofanyika leo Juni 8,2022 Jijini Dodoma.
Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule Kanda ya Magharibi Bi.Edith Mwijage,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki mara baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) kufungua kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na Makao Makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya kilichofanyika leo Juni 8,2022 Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na Makao Makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya kilichofanyika leo Juni 8,2022 Jijini Dodoma.
……………………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda ,amesema elimu bora itapatikana na kuhakisi mahitaji ya nchi endapo kama Maafisa Uthibiti Ubora watakuwa wanaharakati wa mabadiliko katika maeneo yao ya kazi.
Pia amewataka kuhakikisha malezi ya wanafunzi yanapewa kipaumbele ili kutengeneza kizazi bora kwa sasa na baadaye.
Waziri Mkenda amesema hayo leo Juni 8,2022 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya utendaji kazi idara ya uthibiti ubora wa shule kati ya viongozi, uthibiti ubora wa shule na Makao Makuu, ithibati ya shule na wathibiti ubora wa shule wakuu kanda na wilaya.
Amesema Wathibiti ubora wana nafasi kubwa katika kusimamia ubora wa elimu inayotolewa na kuwataka kuendelea kujiongeza katika utendaji kwani wao ndio mboni ya jicho la elimu nchini.
Amewataka wathibiti ubora kote nchini kusimamia kwa weledi zaidi ubora wa elimu kwani wao ni moyo na injini ya elimu.
“Ninyi ni mboni wa elimu hapa nchini, manatakiwa kupambana mambo yakiwa hayaendi vizuri, tizameni kinachoendelea huko katka maeneo yenu ya kazi Serikali imeboresha mazingira ya utendaji wenu jitoeni tuendelee kujituma,”amesema Prof. Mkenda
Aidha amesema kuwa kutokana na Utandawazi na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ni vizuri kujua namna ya kuendana nayo ili watoto wawe na malezi mazuri.
“Malezi ni pamoja na kujali afya za watoto, tushiriki kuhakikisha tunasimamia ujenzi wa vyoo katika maeneo yetu, halmashauri zitenge fedha kujenga vyoo ili changamoto hiyo iweze kuisha”, ameongeza Prof. Mkenda
“Nimeongea na Waziri mwenzangu Mhe. Dorothy Gwajima tupitie miongozo yote watoto wanaaza shule wakiwa wadogo hapa suala la malezi ya mtoto katika maadili ni muhimu,” ameeleza Prof. Mkenda
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji Prof James Mdoe,amesema kuwa Wizara ya Elimu kwa sasa inaendelea na mapitio yaSera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 hivyo amesema wathibiti ubora ni wadau muhimu katika hilo hivyo ni muhimu wakashiriki katika kutoa maoni ya kuboresha sera kwa kuwa wanathibiti ubora wa elimu nchini.
“Kuna zoezi muhimu sana linaendelea la kupitia mitaala na sera ya elimu na mafunzo hivyo wathibiti ubora wanapaswa kushiriki kwa kina katika zoezi hilo kw kiwango kikubwa kwani haitakuwa na maana kama msiposhiriki” amesema Prof.Mdoe
Awali Mkurugenzi wa Idara ya Uthibiti ubora wa Shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi.Euphrasia Buchumu amesema idara hiyo ina jukumu kubwa ambalo kuangalia viwango vya utoaji elimu nchini.
Ametaja baadhi ya mafanikio ya idara hiyo kuwa ni kubadili mfumo wa uthibiti ubora kutoka kuwa ukaguzi kuwa uthibiti, ujenzi wa Ofisi 55 zimejengwa ambazo zimeongeza ari ya utendaji kazi.
Hata hivyo Buchuma,ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23 idara pamoja na mambo mengine inatarajia kuweka Mfumo wa kielektoniki ili kutoa taarifa vizuri, Kuimarisha ikama na Kujengea uwezo wathibiti ubora wa shule.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wathibiti Ubora wa Shule,Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule Kanda ya Magharibi Bi. Edith Mwijage ,amemuhakikishia Waziri Mkenda kuwa watahakikisha wanatekeleza yale yote aliyowaambia ili elimu iendelee kuwa bora