***************************
NJOMBE
Mzee Joseph Gendamwene anaekadiriwa kuwa umri wa miaka 80 mkazi wa Kijiji cha Madobore Kata ya Luponde Wilayani Njombe Amedai kucheleweshwa kufa kutokana na kushindwa kutatuliwa kwa mgogoro wa Ardhi yenye ukubwa wa ekari 1026 Uliopo baina ya wakazi wa kijiji cha Madobole na Shirika la Watawa la Imiliwaha.
Katika siku ya kwanza ya mkutano wa hadhara uliyoitishwa na mkuu wa wilaya ya Njombe wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi katika kijiji cha Madobole mzee Gendamwene anasema anavielelezo vyote vya umiliki wa maeneo yalichukuliwa na masista kwasababu katika kipindi hicho alikuwa kiongozi wa kitongoji ,hivyo anaomba mkuu wa wilaya ya kufatilia mgogoro huo kwa kina na haki ipatikane.
Utata wa eneo hilo ukamfanya mkuu wa wilaya kufunga safari siku ya pili katika kijijii hicho ambapo bado mzee Gendamwene akafika na nyaraka zote za umiliki wa eneo hilo na kuzitoa mbele ya mkuu wa wilaya ambapo anasema pindi mgogoro huo utakapomalizika atafariki dunia kwa amani.
Mara baada ya kujipa muda wa kusikiliza upande zinazosigana ,Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa akaeleza changamoto alizobaini katika umiliki huo na kisha kutoa agizo kwa maafisa ardhi kwenda kufanya tathimini ya eneo lenye mgogoro huku pia akiwataka wananchi na shirika la masista kuwa tayari kwa matokeo.
Wakitoa ufafanuzi juu ya uhalali wa umiliki wa eneo hilo kupitia kwa Sister Maria Nyika wanasema wao wana hati ya eneo hilo waliyopewa na serikali lakini wanampongeza mkuu wa wilaya kwa kutoa nafasi ya kukaa na pande zote mbili.