Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo wilayani hapo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Allan Augustin o Mrema amesema Sumukuvu imekuwa ikiathiri zaidi mazao ambayo ni sehemu ya chakula chetu hapa nchini hivyo basi tunapaswa kuzingatia mikakati ya kukabiliana na changamoto ya sumukuvu ili vyakula viendelee kuwa salama kwa muda wote.
Amesema kupitia mafunzo hayo ambayo TBS wameyakusudia kuyatoa kwa wahusika yatasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na sumukuvu na hivyo kuzalisha na kuuza bidhaa ambazo ni salama.
“Niwapongeze TBS kupitia Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania -TANIPAC kwa kutoa kipaumbele katika suala la kuelimisha jamii ya Wilaya ya Sengerema juu ya usalama wa chakula hususan katika kudhibiti Sumukuvu ili kuweza kukabiliana na tatizo hili”. Amesema Mrema.