***********************
Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
Juni 5
TAASISI Ya Kifedha Ya NMB ,Tawi la Kibiti Mkoani Pwani ,kwa kuunga mkono jitihada za Serikali kuhusiana na Zoezi la sensa linalotarajia kufanyika agost 23 mwaka huu, wametoa vifaa kadhaa na matshirt yenye ujumbe wa SENSA, kwa madiwani wa Halmashauri ya Kibiti .
Akimkabidhi Mwenyekiti na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ,Meneja wa NMB Kibiti Raphael Mbuya alisema ,suala la sensa Ni la Kitaifa ambapo itasaidia kujua idadi ya wananchi na kuiwezesha Serikali iweke mipango mizuri ya kimaendeleo.
Alisema ,bank hiyo inahudumia watu ambao ndio wateja wao hivyo Basi itawasaidia kutambua maeneo na idadi ambayo bado hawajaifikia kutoa huduma.
“Suala la sensa ni muhimu kwetu,kujua tupo wangapi na kujua tulipokosa kupafikia ili tuangalie uwezekano wa kufika”alifafanua Mbuya.
Mbuya alitumia fursa hiyo ,kuiomba jamii ijitokeze na kuwa tayari kuhesabiwa na kushirikiana na Serikali kukamilisha Zoezi hilo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza huduma ya mikopo, anasema wanatoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo,wa kati na wakubwa , Vilevile waajiriwa wa Serikali,sekta binafsi ,wastaafu ,wakulima na wafugaji.