Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunuku vyeti wahitimu katika Mahafali ya Hamsini na Mbili kwa Minajili ya Kutunuku Digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada za Uzamili na Digrii za Awali katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na Mbili kwa Minajili ya Kutunuku Digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada za Uzamili na Digrii za Awali katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Mstaafu Mhe.Damian Lubuva akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na Mbili kwa Minajili ya Kutunuku Digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada za Uzamili na Digrii za Awali katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye mahafali ya Hamsini na Mbili kwa Minajili ya Kutunuku Digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada za Uzamili na Digrii za Awali katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimepiga hatua katika miradi mikubwa ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu .
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka UDASA mpaka zilizopo ofisi za Kurugenzi ya Miliki, ukarabati wa mabweni ya wanafunzi na kukamilika kwa ujenzi wa Tenki la Maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita laki tano (500,000) za maji.
Amayasema hayo leo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye katika Mahafali ya Hamsini na Mbili kwa Minajili ya Kutunuku Digrii za Uzamivu, Umahiri, Stashahada za Uzamili na Digrii za Awali katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Amesema katika miradi hiyo pia wanaendelea na ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia, kuanza ujenzi wa Maabara Kuu ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kuanza ujenzi wa Shule Kuu ya Uchumi na kuendelea na ukarabati wa Maabara za Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi.
Aidha amesema Chuo Kikuu kiliongeza Fedha za Utafiti na Ubunifu kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani ambapo katika mwaka wa fedha 2020/2021, Chuo b kilitenga Shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya utafiti na ubunifu.
“Kiwango cha fedha kiliongezeka hadi shilingi Bilioni 3.15 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Fedha zote hizi ziligawiwa kwa wanataaluma waliowasilisha mapendekezo ya utafiti na miradi mbalimbali ya ubunifu”. Amesema Prof.Anangisye.
Pamoja na hayo Prof.Anangisye amesema kwa mara kwanza Chuo hicho idadi ya wanawake waliopata shahada ya Uzamivu ni wengi zaidi kuliko wanaume ikiwa ni asilimia 53 ya wahitimu 68.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji Mstaafu Mhe.Damian Lubuva amesema baraza linawasisitizia wanataaluma kufanya bidii katika kufanya tafiti kwenye maeneo yatakayogusa maisha ya watanzania ili tafiti hizo zigoe majibu ya matatizo yaliyoko kwenye jamii.
Amesema baraza liko macho kuhakikisha kuwa sera na miongozo mbalimbali inayopitishwa inafanyiwa kazi kwa kuzingatia malengo makuu ya Chuo.