Mkuu wa Sehemu ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Bwana Anyitike Mwakitalima akipitia ramani za mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini unaotekelezwa katika Kituo cha Afya Kinyambuli Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida
kuu wa Sehemu ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Bwana Anyitike Mwakitalima akielekeza jambo kwa wasimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini unaotekelezwa katika Kituo cha Afya Kinyambuli Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida
Mkuu wa Sehemu ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Bwana Anyitike Mwakitalima akielekeza jambo kwa wasimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini unaotekelezwa katika Kituo cha Afya Kinyambuli Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida
Muonekano wa nje wa vyoo sita vinavyojengwa katika kituo cha afya Kinyambuli Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida chini ya mradi wa huduma endelevu za maji na usafi wa mazingira vijijini
Muonekano wa nje wa Tanki la kuvuna maji ya mvua linalojengwa katika kituo cha Afya Kinyambuli, Halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida
…………………………………..
Na. WAF, MKALAMA -SINGIDA
Mratibu wa Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Bwana Anyitike Mwakitalime ametoa wito kwa Mkandarasi wa Halmashauri ya Mkalama iliyoko mkoani Singida kusimamia kwa karibu mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini ili kukamilika kwa viwango vilivyo bora na mradi kuanza kutoa huduma kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mwakitalime ametoa rai hiyo leo wakati akifanya ukaguzi wa mradi huo ambapo amesema ipo haja ya mkandarasi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama kuwa karibu na mafundi pamoja na wasimamizi wa mradi huo ili kuhakikisha kila hatua inayofikiwa basi inakuwa imedhibitishwa na mkandarasi na mradi huo kukamilika kwa ufanisi unaohitajika.
“Mradi huu katika kituo cha Afya cha Kinyambuli kilichopo kata ya Kito wilaya ya Mkalama unafanya kazi kubwa mbili za ujenzi wa tanki la kuvuna maji ya mvua lenye ujazo wa Lita 100,000, sambamba na usambazaji wa maji kwenda katika maeneo muhimu ya kutolea huduma hapa kituoni pamoja maeneo ya vyoo na sehemu za kunawa mikono”, ameeleza Mwakitalime
Vile vile Mwakitalime amesema kuwa mradi huo wanajenga matundu sita ya vyoo ambapo matundu matatu ni ya wanawake, mawili ni ya wanaume na moja ni kwajili ya watu wenye ulemavu.
Pia ameeleza kuwa mradi unajenga minara miwili ya kuweka matenki ya maji kwa ajili ya kusambaza maji ili kuongeza kasi ya usambazaji maji katika sehemu muhimu za kituo hicho.
“Mradi huu umekuja baada ya kufanya tathimini katika kituo hiki mwaka jana na kubaini kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa maji katika kituo hiki”, amesema Mwakitalime.
Aidha, Mwakitalime amewapongeza uongozi wa Kituo hicho kutokana na kasi ya utekelezaji wa mradi inaenda vizuri na inaridhisha kwa ubora unaohitajika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kituo cha Kinyambuli, Mzee Samweli Mlilo amesema kwa niaba ya wananchi wa kata cha Kito wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluh Hassan kwa kuwaletea mradi wa huduma endelevu za maji na usafi wa mazingira vijijini ambao utakwenda kutatua changamoto mbalimbali katika kituo cha afya na kufanya huduma za afya ziboreke Zaidi.
“Sisi kama wanachi wa Kito jukumu letu kubwa ni kuhakikisha tunasimamia kwa karibu mradi huu unakamilika na kuutunza vema ili mradi huu uweze kuwa na tija kwenu wanaKito”, amesisitiza Mzee Mlilo.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Manunuzi Kituo cha Afya Kinyambuli, Marter Lazaro ameeleza kuwa wakina mama wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kutokana na changamoto ya maji hivyo ujio wa mradi huo utakwenda kuleta nuru kwa wakina mama wa Kito pindi mradi utakapo kamilika na kuanza kutoa huduma.