Mkurugenzi wa BOT tawi la Arusha,Charles Yamo akizungumza katika mkutano huo Jijini Arusha .(Happy Lazaro)
…………………………………….
. .
Happy Lazaro, Arusha.
Arusha. ZAIDI ya Wataalamu 400 wa maswala ya fedha nchini kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha wamepatiwa elimu ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma za kifedha ili kuleta ufanisi zaidi maeneo yao ya kazi.
Mkutano huo wa siku tatu umewashirikisha watalaamu hao kutoka taasisi mbali mbali za kifedha zikiwemo mabenki, wahasibu, wakaguzi, maofisa wa bima na mapato “TRA”.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania, Pius Maneno akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo amesema kuwa, wanalenga kuwaelimisha zaidi wataalamu hao juu ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma ambayo ni rahisi na yenye ufanisi zaidi ili kuendana na Kasi ya mapinduzi ya nne ya viwanda.
“Hapa tuna mada 11 tunazo elekezana zaidi ni matumizi ya mtandao katika kutoa huduma zetu za kifedha ikiwemo utoaji wa taarifa sahihi za kifedha na namna ya kuzuia viatarishi vya kuzuia malengo yetu” amesema Maneno.
Maneno alisema kuwa wanatarajia pia kuwanoa washiriki wao katika kutambua mbinu za masoko ya kazi zao, maswala ya Kodi, utawala Bora, jinsi ya kuandaa na kuandika taarifa za kuripoti maswala ya fedha lakini pia kukumbushana majukumu ya wahasibu na Benki Kat utoaji wa taarifa za fedha haramu zinapojitokeza.
“Lengo la haya yote ni kufanya wataalam wetu wajue majukumu yao, lakini kutumia Tehama katika kuhudumia jamii ambayo itarahisisha kazi, itawafikia wananchi wengi kwa Bei nafuu na itapunguza umaskini kwa kukuza uchumi”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania “BOT” tawi la Arusha, Çharles Yamo alisema kuwa mafunzo haya wamekuwa wakiyatoa ili kuwafanya wataalam hao waendane na kasi ya dunia kwenye mapinduzi yaliyopo katika utoaji wa huduma za kifedha.
“Katika mkutano huu kubwa ni mapinduzi ya nne ya viwanda katika matumizi ya Tehama, katika ukuaji wa uchumi wa uchumi wa jamii na nchi na nchi kwa ujumla wake”
Alisema kuwa wanasisitiza pia maadili katika utoaji wa huduma na wahusika wa kibenki wawe wanatoa taarifa sahihi za mikopo yao na riba lakini pia wakopaji katika taasisi zao ili kupunguza tatizo la mikopo chechefu.
“Tunawasisitiza pia taaisis wa kibenki wawe wanatoa taarifa sahihi za wakopaji wao ili zisaidia taasisi zingine kuzipata na kutumia dhidi ya wateja wanaokwenda kukopa pengine na kujiridhisha endapo mkopo huo hautawaathiri, hiii itasaidia kupunguza mikopo chechefu kwa wateja lakini pia heshima kwa Benki”
Yamo alitumia nafasi hiyo kuwaonya taasisi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo mitaani bila leseni ya kufanya biashara hiyo wala kibali cha BOT kuwa watawachukulia sheria.
“Pia niwaombe mabenki watoa mikopo kwa riba elekezi ya Serikali isiyozidi asilimia 15 kwa mikopo mikubwa ya mda mrefu Hadi asilimia saba ili kuleta maana ya kuwasaidia wananchi wakopaji na sio kuwakandamiza”