**********************
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Mkuu wa Mkoa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewataka watalaam wa afya Mkoani hapo kutumia utaalamu wao na kuja na Mikakati ili kuleta matokeo katika kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Kunenge ameyasema hayo Mei 30, 2022 wakati akifungua kikao kazi cha Wataalamu na Wadau wa Utekelezaji wa Mradi wa KOFIH Wilayani Bagamoyo ukumbi wa Millennium beach Resort
Kunenge amewataka Wataalamu hao kushirikisha Wananchi katika uaandaaji wa mipango yao.
“Lazima mjipange mumize Vichwa tupate Mikakati yenye matokeo chanya” alisema Kunenge.
Kunenge amewaeleza kuwa tayari “Matarajio yanafahamika katika Sera na ilani ya chama cha mapinduzi nini kifanyike kufikia malengo hayo ni kazi yenu Wataalamu” alisema Kunenge.
Kunenge ameeleza kuwa kupitia mradi huo Mkoa umeweza kupunguza Vito vya akina mama vitokanavyo na uzazi toka 82 mwaka 2015 hadi 51 mwaka 2021 na vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 887 mwaka 2015 hadi 392 mwaka 2021.
Kunenge amewashukuru wadau hao kuwa kuongeza mwaka mmoja wa Mradi na kufanya mradi huu kuwa wa miakw 7 na wameongeza kiasi cha pesa toka dola za kimarekani 3,000,000 kufikia dola 4,900,000.
Awali akizungumzia faida mbalimbali zilizotokana na mradi wa KOFIH Mkoani Pwani mganga mkuu Dr Guni Kamba amesema wameweza kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Wataalam watoa dawa za usingizi, Ujenzi wa vyumba vya upasuaji, vifaa tiba, ambulance na kujengewa wadi za wagonjwa,
Pia mwakilishi wa wizara Dr.Phineas sospiter amelishukuru Mradi wa KOFIH Kwa kuisadia wizara kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Naye Mr Seungrae Ha Mwakilishi KOFIH Tanzania amesema kwa pamoja tumeweza kukuza huduma za Afya Tanzania, na wamekutana kwenye kikao hicho kufanya Tathimin ya Mradi kwa miaka 6 iliyopita na kupanga mipango ya Utekelezaji kwa mwaka ujao.
Kikao hicho kilihudhuriwa na madaktar Wakuu wa Wilaya timu za usimamizi wa Afya za Wilaya wawakilishi kutoka Mikoa ya Pwani, Dodoma na Morogoro. Kwa Mkoa wa Pwani Mradi huu unatekelezwa katika Halmshauri 6 za Mkoa huo