Na Mwandishi Maalumu,Acrra-Ghana
Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, Wenye Uwakilishi Sambamba nchini Ghana, umefanya Kongamano la Utalii, Uwekezaji na Biashara (Tanzania-Ghana Tourism, Investment and Trade Forum (TN-TITF), Mei 28, 2022, ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Nigeria, wenye Uwakilishi Sambamba nchini Ghana, umefanya Forum ya Utalii, Uwekezaji na Biashara (Tanzania-Ghana Tourism, Investment and Trade Forum (TG-TITF), Jijini Accra, Ghana.
Jukwaa hilo lilikusudia kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania Bara na Zanzibar, fursa na vivutio vya uwekezaji pamoja fursa za biashara. Jukwaa hilo liimefunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, ambapo pia limehudhuriwa na wadau wa sekta hizo kama vile Jumuiya za Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, Kilimo na Madini za Ghana, Makampuni ya Utalii, Wafanyabiashara na Wawekezamitaji.
Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, na Madini ya Ghana, Clement Osei-Amoako.
Aidha, Taasisi za Jamhuri ya Muungano, hususani TTB, TIC, ZIPA, EPZA, TanTRADE, Jumuiya za Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, Kilimo na Madini za Tanzania Bara na Zanzibar, zilishiriki na kuelezea kwa undani fursa, miundo, majukumu na nafasi zake katika kukuza Biashara, Utalii na Uwekezaji nchini Tanzania.
Pamoja na mambo Mengine, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria anbaye pia anawakilisha nchi ya Ghana Dk. Benson Bana, alieleza kuwa Jukwaa hilo linakusudia kuleta taasisi, jumuiya za wafanyabiashara, wawekezaji wa Tanzania na Ghana kuona namna ya kushirikiana na kukuza mahusiano ya uwili baina ya nchi hizi, ambazo uhusiano wake ulianzatangu kipindi cha waasisi wa mataifa haya, Mwl. Julius Nyerere na Kwame Nkrumah, Marais na Baba wa Mataifa ya Tanzania na Ghana mtawalia.