Silvia Amandius,Muleba.
Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Muleba Dr.Leontine Rwamulaza amewaaagiza watumishi wote wa afya katika wilaya ya muleba kuendelea kutoa huduma ya afya kwa gharama pungufu kwa watu wenye ulemavu kwa kutumia busara huku wakisubili muongozo,Sera na kanuni.
Akizungumza katika kikao Cha tathimini Cha uondoshwaji wa vikwazo vya afya kwa watu wenye ulemavu kilichofanyika muleba katika ukumbi wa Suzana hotel ambapo amesema bado halmashauri inasubili miongozo,Sera na kanuni ili kuweza kuwahudumia kwa ubora kulingana na hali zao walizo nazo.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa bado wanayo fursa hata watu wenye ulemavu kuendelea kuwakumbusha viongozi wa ngazi ya mkoa kuona Ni kwa namna gani watawezesha na kushughurikiwa katika upande.
Pia nae mwenyekiti wa watu wenye ulemavu mkoa wa Kagera ndg. Laulian Pancaras ameiomba serikali ya wilaya na mkoa kuendelea kuifanyia kazi Sera ya mtu mwenye ulemavu kutibiwa bure au kwa gharama nafuu kwani Sera,kanuni na miongozo ishaelekezwa kutoka serikali kuu na bado miongozo hiyo aijafanyiwa kazi.