Na Silvia Mchuruza,Bukoba
Halmashauri ya manispaa ya Bukoba mkoani kagera imekabidhi hundi za shilingi milioni 139 kwa vikindi vya akina mama na watu wenye ulemavu lengo likiwa Ni kuwainua kiuchumi.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano hayo meya wa manispaa ya Bukoba mh. Godson Rwegasila Gibson iliyofanyika katika ukumbi wa Bukoba sekonda uliopo manispaa ya Bukoba mkoani kagera amewataka wanavikundi wote waliokabidhiwa mikopo kuhakikisha wanaitumia vizuri ili kuepukana na matumizi mabaya ambayo yanaweza kujitokeza.
Pia amewasisitiza vijana kuhakikisha wanakuwa waaminifu na kulejesha kwa wakati kwani ndilo kundi linalotajwa kutokuwa na muitikio zaidi na kusumbua katika urejeshaji wao ambapo amesema atowafungia macho katika kulejesha mikopo hiyo kwani wanapewa miezi 3 ya matazamio.
Aidha nae afisa ustawi wa jamii ndg Wanchonke Chinchibera ametoa Rai kwa vikindi vya watu wenye ulemavu pamoja na vijana kuhakikisha wanakuwa na muitikio ili kuweza kuongeza makundi yao ili waweze kukopeshwa wengi zaidi.
Kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022 manispaa ya Bukoba imetoa kiasi Cha shilingi Milioni 312 kwa vikundi Kati ya vikundi hivyo vikundi vya wanawake Ni 46 vyenye wanachama 386 ambavyo vilipokea shilingi milioni 231, wenye ulemavu vikundi 4 venye wanachama 20 ambapo vilipokea milioni 13, na vijana 9 vyenye wanachama 57 ambapo vilipokea Milioni 68.
Nao baadhii ya wanavikundi akiwemo ndg.disiraus kisimbazi kutoka kundi la watu wenye ulemavu ameshukuru na kusema kuwa mikopo hiyo waliopokea watahakikisha wanarejesha kwa wakati na itawasaidia kuwainua kiuchumi.