Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na baadhi ya viongozi wa
chama cha mapinduzi wakipita katika barabara ambayo inatarajiwa kujengwa
kwa rami kutoka Iringa Mjini hadi hifadhi ya taifa ya Ruaha.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewahakikishia watalii kuwa barabara
ya Iringa hadi hifadhi ya taifa ya Ruaha itajengwa kwa lami kwa kuwa benk ya
dunia imeshakubari na imeshatoa fedha za ujenzi.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kitalii ya kamati za siasa za wilaya ya Iringa vijijini na
manispaa ya Iringa Moyo alisema kuwa Serikali na benk ya ipo tayari kuhakikisha
mwaka huu kwa ajili ya kurahisisha usafiri kufika katika hifadhi ya taifa ya
Ruaha.
Moyo
alisema kuwa lengo la Serikali na benk ya dunia ni kuhakikisha wanakuza utalii
wa nyanda za juu kusini kupitia hifadhi ya taifa ya Ruaha ambayo imekuwa na
vivutio vingi ambayo kila mtalii anatamani kuvitembelea.
Alisema kuwa Serikali ya wilaya ya Iringa imeacha shughuli zote ambazo walizipanga
kuzifanya kando kando ya barabara hiyo ili kupisha ujenzi wa barabara ambayo
inamanufaa makubwa kwa wananchi wa Iringa na taifa kwa ujumla.
Moyo
aliwaomba wananchi wote ambao barabara hiyo inawapitia kutoa ushirikiano kwa
wakandarasi ambao watakuwa wanajenga barabara hiyo.
Alisema
kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kutasaidia kukuza uchumi wa
wananchi wa wilaya ya Iringa na taifa na kuleta maendeleo kutokana kuongezeka
kwa watalii katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Manispaa ya Iringa Saidi Rubeya
alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami
kutasaidia kukuza utalii kwa wananchi wa Iringa.
Rubeya
alisema kuwa changamoto ya barabara hiyo kunasababisha kupunguza watalii wazawa
kutokana na kushindwa kufika hifadhi ya taifa ya Ruaha kwa kutumia magari yao
madogo ambayo wananchi wengi wanayo.
Alisema
kuwa anapenda kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuvitangaza vivutio vingi vya utalii
vilivyopo nchini Tanzania.
Rubeya
alisema kuwa ziara ya Royal Tour imeleta mafanikio makubwa na itaendelea kuleta
neema kwa wananchi na taifa kwa kuongeza wawekezaji na watalii ambao
watachochea maendeleo ya nchini.
Naye
mwenyekiti wa wilaya ya Iringa vijijini wa chama cha mapinduzi (CCM)Costantino
Kiwele alisema kuwa wanapongea hatua
ya mkuu wa Wilaya kuwawezesha kutembelea hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa
nchini, Wakiweka bayana kuanzia sasa wao ni mabalozi rasmi ya hifadhi hiyo ya
taifa
Kiwele alisema kuwa baada
ya kufanya utalii kwenye vivutio ya hifadhi ya Ruaha watakuwa mabalozi wa
hiyari kuvitangaza vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo.
Alisema kuwa hifadhi hiyo
imekuwa inamchango mkubwa kwa jamii kutokana na fedha inayoingiza kusaidia
katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo kwa wananchi.
Kiwele aliongeza kuwa
hifadhi ya Ruaha imekuwa chachu ya kuutangaza mkoa wa Iringa na Tanzania kwa
ujmla hivyo wanaunga mkono alichokifanya Mheshimiwa Rais kwenye Royal Tour
ambayo imeanza kuleta neema kwa watanzania