WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa,akizungumza wakati akifunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara/ Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichomalizika leo Mei 27,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara/ Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichomalizika leo Mei 27,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa, wakati akifunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara/ Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichomalizika leo Mei 27,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara/ Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichomalizika leo Mei 27,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro ,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara/ Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichomalizika leo Mei 27,2022 jijini Dodoma.
……………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali itaendelea kusimamia Watumishi wa Umma kufanya kazi kwa nidhamu na uwajibikaji wakati wa kuwahudumia wananchi.
Kauli hiyo ameitoa leo Mei 27, 2022 Jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara/ Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma lengo likiwa ni kuwajengea uwezo, kufuata taratibu za kazi na kuwa na ubunifu katika maeneo yao ya kazi.
“Tufahamu mishahara yetu inatokana na wananchi, wajibu wako kama mkuu wa Idara ya utawala na rasilimali watu ni kutekeleza wajibu wako kwa watumishi ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi na hilo ndio lengo la Serikali” amesema Waziri Bashungwa
Bashungwa amewaelekeza Maafisa utumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwasadia Wakuregenzi katika kutekeleza na kufanya maamuzi ya kiutendaji katika halmashauri zao “ninyi mna mamlaka ya kumshauri Mkurugenzi kufanya maamuzi sahihi ya kiutumishi timizeni wajibu huo kwa kutenda haki”
“pamoja na kusimamia maadili ya utumishi wa umma pia mna wajibu wa kusimamia miradi ya maendeleo kwasababu inatekelezwa na watumishi, tukifuatilia utendaji kazi katika maeneo yenu na kukuta changamoto, afisa utumishi utawajibika sababu unakuwa umeshindwa kusimamia kazi yako ya rasilimaliwatu” amesisitiza Waziri Bashungwa
Aidha, Bashungwa amemuelekeza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI kufanyia kazi suala la watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kukaimu nafasi mbalimbali kwa muda mrefu, kulifanyia kazi kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni za kiutumishi iliwaweze kushika nafasi hizo na kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Kwa upande wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka maafisa utumishi kuangalia kero za utumishi amesema zipo changamoto zinatokea katika maeneo yao ya kazi mtumishi hapati huduma mpaka anapeleka kero zake kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi hilo halikubaliki amewataka kujielekeza kwenye utendaji kazi kwa kufuata sheria na haki katika kufanya maamuzi.
Naye Mwenyekiti wa Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Bi. Tabia Mohamed ametoa kwa kuwepo kwa kikao hicho ambacho l kinasaidia kuwakumbusha majukumu yao pia kujifunza utumiaji wa mfumo mpya wa kuweka taarifa za watumishi ambapo wao ndio walengwa wa utumiaji wa mfumo huo amesema, mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) utawasaidiawa kuweka taarifa sahihi za watumishi na kupima uwajibikaji.
Kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kiliendana na kauli mbiu inayosema “Utumishi wa Umma wenye Uadilifu, Nidhamu, Ubunifu, Weledi na Uwajibikaji wa Hiari kwa Ustawi wa Jamii”