Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza Frank Mkilanya akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2022 kwa waandishi wa habari
…………………………………………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Katika kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inatekelezwa kwa uaminifu na kwa kiwango kinachotakiwa,Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2022 imefanya ukaguzi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 17 yenye zaidi ya bilioni 25.
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa Mei 27,2022 na Mkuu wa Taasisi hiyo Frank Mkilanya,wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa waandishi wa habari.
Mkilanya amesema kati ya miradi hiyo 17 iliyokaguliwa miradi 6 ni ya elimu ambayo ilihusisha ujenzi wa matundu ya vyoo,ujenzi wa vyumba vya madarasa, miradi 8 ilihusu ujenzi na ukarabati wa barabara,mradi mmoja ni wa ujenzi wa stendi ya mabasi nyegezi na miradi 2 ni ya ufuatiliaji wa fedha za Uviko kwa Wilaya ya Nyamagana na ngazi ya Mkoa.
“Pamoja na miradi hiyo iliyokaguliwa Takukuru Mkoa wa Mwanza imeweza kufanya uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa mapato yatokanayo na madini ya ujenzi,uchambuzi wa mfumo wa mianya ya rushwa katika utoaji elimu ya ugani kwa wakulima,uchambuzi wa mfumo na mianya rushwa katika utekelezaji wa shughuli za chanjo ya Uviko-19”,amesema Mkilanya
Amesema kupitia chambuzi za mifumo zilizofanyikakwenye maeneo mbalimbali,kunachangamoto ndogo zilizobainika na wameisha Kaa kwenye vikao kwa lengo la kuwekeana maazimio na makubaliano ya pamoja kwaajili ya utekelezaji kwa yote yaliyobainika ili kuweza kuboresha mifumo na utoaji huduma.
Mwisho ametoa wito kwa Wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza waendelee kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ili kuweza kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa sheria.