*****************************
Na Silvia Mchuruza.
Muleba,Kagera
Uongozi wa shule ya msingi kagondo B iliyopo kata ya muhtwe wilaya ya muleba umeiomba serikali kuwaboreshea miundombinu ya shule ikiwemo kuwapatia walimu,vifaa vya kufundishia na kuwa ujenzi wa bwalo la chakula.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa shule hiyo Bi Estar Rwantoga ambae pia ni mwalimu wa elimu maalumu amesema kuwa shule hiyo inao wanafunzi ambao ni jumuishi wakiwemo wenye ulemavu waliogawanyika makundi manne wakiwemo wenye ulemavu wa viuyngo 12, viziwi 24,uoni hafifu 3 na wenye ulemavu wa akili 40 ambapo amesema licha ya kuwa na watoto hao wenye ulemavu bado wanayo changamoto kubwa ya walimu kwani yeye ndiye mwalimu pekee wa elimu maalumu.
“Kiukweli tunapata shida Sana tunao Watoto wenye ulemavu kwa makundi tofauti ambao jumla Ni 79 na Mwalimu ni Mimi peke yangu ndiyo maana nalazimika kuwaambia walimu wengine nao wafundishe ata Kama Awana mafunzo ya elimu maalumu hii yote Ni kutokana na changamoto na walimu”
Aidha pia mwl.Ester ameongeza na kuiomba serikali pamoja na wadau wa elimu jumuishi kuitazama shule hiyo kwani licha ya changamoto hiyo bado shule hiyo mazingira yake siyo rafiki kwa Watoto hao kwa upande wa bwaro la chakula na hata jiko linalotumika kupika chakula Chao.
Hata hivyo nap baadhi ya Walimu akiwemo Mwalimu Kabura Nestory amesema kuwa licha ya kuwepo kwa kwa mafanikio ya serikali kuwajengea bweni ambalo limegharimu million 80 lakini bado alijakamilika kutokana na fedha kuisha lakini bado serikali inajitaidi kuhakikisha bweni linakamilika lakini wao Kama Walimu ambao Awana mafunzo ya elimu maalumu bado wanapata changamoto katika kuwafundisha Watoto hao.