MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo akizungumza wakati wa warsha hiyo kulia ni Meneja Mkuu wa Amend Tanzania Simon Kalolo |
Meneja Mkuu wa Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza wakati wa warsha hiyo |
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga akizungumza wakati wa warsha hiyo |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
ASILIMIA
76.14 ya tabia za kibinadamu zimetajwa kama mojawapo ya vyanzo vikuu
vinnne ambavyo vinasababisha ajali za barabarani na hivyo kupelekea
kupoteza maisha au kupata majeraha ikiwemo kupoteza mali.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO)
Leopord Fungu wakati warsha ya utoaji wa taarifa pamoja na kupata maoni
kutoka kwa wadau wa usalama barabarani iliyoandaliwa na Taasisi
isiyokuwa ya kiserikali ya Amend.
Ambapo alisema ni vyema
watumiaji wa vyombo vya moto na watumiaji wengine watumie matumizi
sahihi ya bara bara ili kuepusha athari mbalimbali ambazo wanaweza
kuzipata ikiwemo ajali zinazotokana na kutokuwa makini.
Fungu
alisema tabia hizo za kibinadamu zimesababisha kupelekea kwa asilimia
kubwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa na kama vitazingatiwa ajali
zitapungua na hivyo kuondokana na ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa
zikiondoa nguvu kazi ya Taifa.
“Madereva kuendesha vyombo vya
moto bila mafunzo ya usalama barabarani hii sio sawa na wengi wanapenda
nyia za mkato kujifunza na tabia hizo tukiziacha zitatusaidia kupunguza
ajali “Alisema RTO huyo.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa
serikali,watendaji wakiwemo madiwani katika maeneo yao kama kuna watu
wanaoendesha boda boda wahakikishe kwamba wanakuwa wamepata elimu ili
kuwapeusha na ajali.
Awali akizungumza Mstahiki Meya wa Jiji
la Tanga Abdurhaman Shiloo alitoa wito kwa wafanya biashara katika
halmashauri ya jiji la Tanga ambao wanatumia barabara kuweka bidhaa zao
kuacha mara moja kufanya hivyo.
Meya huyo alisema vitendo
hivyo sio sawa hata kidogo lazima waheshimu taratibu zilizowekwa ikiwemo
kuacha kupanga bidhaa zao kwenye maeneo ya maegesho ya barabara na
kuvuka milango mlikodishwa na kuweka barabarani ambazo ni matumizi ya
vyombo vya moto.
“Wapita njia tafadhali msitumie njia za watumia
kwa miguu kuweka bidhaa zenu lakini tiini sheria bila kushurti kwa
kuziiondoa bidhaa hizo kila mtu ajue mipaka ya milango wake na bidhaa
zilizoingia barabara kuacha mara moja kwa lengo la kuepukana na ajali
zinazoweza kujitokeza“Alisema
Awali akizungumza wakati wa warsha
hiyoMkurugenzi Mtendaji wa Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Sipora Liana
alisema watatoa wataendelea kushirikiana huku wakiwashukuru kwa
kuendelea kuweka miundombinu kwenye maeneo yote katika Jiji la Tanga.
Alisema
yeye kama mdau iwapo shirika hilo linataka kuweka miundombinu na
bodaboda watengewe maeneo mazuri yatayowezesha kufanya kazi zao vizuri
na waweke mtandao utakaofanya wajulikane pindi linapotokea tatizo.
Hata
hivyo Meneja Mkuu wa Amend Tanzania Simon Kalolo alisema lengo la
warsha hiyo ni kutoa mrejesho wa nini ambacho kimefanyika kwa miaka
mitatu iliyopita wakizungumzia elimu kwa shule za Msingi,Miundombinu.
Alisema
kwamba wameamua kuweka alama kwenye maeneo mengi ya shule katika Jiji
la Tanga ili kuweza kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika .
“Tumekuwa
tukiweka alama za aina mbalimbali barabarani,tumeanza jitihada
mbalimbali kwenye shule zenye mahitaji maalum zinahitaji nguvu zaidi kwa
kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa alama na wamekuwa hawajui”Alisema
Kalolo
Alisema pia kuboresha barabara kuwa rafiki kwa watu
wenye mahitaji maalumu hasa watoto mafunzo ya madereva kwa waendesha
boda boda ambao wamekuwa wakisababisha ajali nyingi nchini na Tanga kwa
hiyo warsha hiyo ilikuwa ni kupata maoni na mapendekezo.
Hata
hivyo alisema baadae ili kuweza kuona suala la usalama barabara linavuka
na kuona waboreshe mipaka iliyozoelekeza kuhakikisha wanatokoeza ajali
za barabarani.