Na Silvia Mchuruza,Bukoba.
Upatikanaji wa fimbo nyeupe kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kutoona bado ni changamoto Jambo ambalo linawafanya kutumia fimbo za miti.
Akizungumza na waandishi wa habari bwana Novath Joseph ambae Ni mtu mwenye ulemavu wa kutoona ambae pia Ni Katibu wa chama Cha watu wenye ulemavu wa kutoona katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba TLB KAGERA ameiomba serikali kuwatazama kwa jicho la tatu kwani fimbo nyeupe bado upatikanaji wake ni mgumu.
“Fimbo zetu hizi nyeupe zinapatikana kwa shida sana na zikipatikana zinauzwa kwa Bei ghari kwani fimbo moja inaweza kuuzwa Hadi shilingi elfo 25 mpaka 30 pesa ambayo unakuta Ni ngumu kupatikana na mwisho wa sikulazimishi mtu anaamua kutumia fimbo za mti ambao pia siyo imara”
Hata hivyo ameongeza kwa kuwaomba wadau wa masuara ya watu wenye ulemavu kwa ujumla ikiwemo na serikali kuwarahisishia Kodi wale watu ambao wanaingiza nchini vifaa vya matumizi ya Aina mbalimbali kwa ajili ya watu wenye ulemavu ili kuwapa hamasa ya kutoa misaaada hiyo zaidi.
Licha ya changamoto hiyo pia ametoa wito kwa watu wenye ulemavu wa kutoona kuendelea kujishughulisha na shughuri mbalimbali katika jamii na kuachana na kujitenga kwani kuwa na ulemavu wa aina yeyote ile siyo sababu ya kumfanya mtu kuwa ombaomba.
” Mimi hapa licha ya kuwa na changamoto mbalimbali za kimaisha lakini bado ninajishughurisha na ujasiliamari wa uuzaji wa kahawa lakini pia mke Wangu anajishughurisha na utengenezaji wa mandazi na bado tunaendesha familia vizuri japo bado Nina changamoto ya mtaji ,lakini hii inanisaidia kuepukana na kuwa ombaomba au kuwa kero katika jamii” Alisema bw.Novath.