Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel ,akizungumza wakati akifungua kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE kilichofanyika jijini Dodoma
Mwenyekiti wa wabunge vinara wa lishe Dustan Kitandula ,akielezea kuwa bado kuna changamoto kubwa kwenye masuala ya lishel icha ya kelele walizopiga wabunge hao kwa miaka mitano wakati wa kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE kilichofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa PANITA Bw.Tumaini Mikindo,akielezea shirika linavyofanya kazi wakati wa kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE kilichofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu kutoka Shirika la Save The Children Dk.Joyceline Kaganda,akielezea utekelezaji wa Afua za lishe endelevu na nafasi za wabunge katika kuboresha lishe wakati wa kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE kilichofanyika jijini Dodoma.
Meneja Mradi USAID Lishe Endelevu kutoka PANITA Bi.Jane Msagati,akitoa taarifa na athari za lishe nchini kwa watoto wakati wa kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE kilichofanyika jijini Dodoma.
SEHEMU ya wabunge wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE kilichofanyika jijini Dodoma.
BAADHI ya wabunge wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE kilichofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na wabunge mara baada ya kufungua kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE kilichofanyika jijini Dodoma
………………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
IMEELEZWA kuwa bado kuna changamoto katika kipaumbele cha lishe huku Serikali ikiowaomba wabunge nchini kupaza sauti zao katika suala la lishe.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel wakati akifungua kikao cha wabunge kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa USAID LISHE
Amesema kuwa wabunge tunawaomba mpaze sauti zenu katika masuala ya lishe ili jamaii ielewe umuhimu wake
‘Kutokana na hilo, Wizara ya Afya imesema ni bora kuja na sheria ya itakayotambua umuhimu wa lishe ili iweze kusimamiwa.’
Mradi huo upo katika mikoa ya Dodoma,Morogoro,Iringa na Rukwa na unatekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo miongoni mwao ni Deloitte,Panita Save the Children
Dk.Mollel amesema kuwa,pamoja na mipango mingi na mizuri inayofanywa na Serikali, lakini suala la lishe halina msukumo ndiyo maana mapambano yake yanakuwa magumu licha ya uzalishaji mkubwa wa vyakula kwenye mikoa mingi.
“Watu wanasema kuwa wanasaidia kwenye lishe lakini ukifuatilia wanalipia vipeperushi kwa karibu Sh7 Milioni wakati tatizo katika eneo husika lilitaka Sh700,000 zingine zinaingia kwenye makongamano, warsha na semina,huo ni usanii,” amesema Dk.Mollel.
Aidha amesema kuwa Watanzania wengi wanachanganya kati ya chakula na lishe wakati ni vitu viwili tofauti hivyo elimu bado inatakiwa ili watambue hilo ili watu wapunguze semina na makongamano na kujitahidi kutenga bajeti ya kusaidia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wabunge vinara wa lishe Mhe.Dustan Kitandula amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa kwenye masuala ya lishel icha ya kelele walizopiga wabunge hao kwa miaka mitano.
‘Inashangaza hata mashule kuona watoto wanaagizwa kupeleka maji kwa ajili ya kunyeshea maua badala ya mboga hivyo elimu inahitajika katika kufanikisha hilo”amesema Mhe.Kitandula
Awali Meneja Mradi USAID Lishe Endelevu kutoka PANITA Bi.Jane Msagati amesema tatizo la lishe linatokana na halmashauri nyingi kutokutilia maanani kwenye suala hilo na hata fedha zinazotakiwa kutengwa hazitengwi na zikitengwa hazipelekwa inavyotakiwa.
Msagati amesema mapambano ya lishe limo hata katika Ilani ya uchaguzi ya CCM hivyo halmashauri kutokutenga fedha ni kufanya kwa makusudi lakini si bahati mbaya.
‘Aliwaomba wabunge kuwasaidia kulisemea jambo hilo kwenye halmashauri kwani bado tatizo ni kubwa hata wilaya ambazo zinazalisha kwa wingi chakula.pembezoni na miji”amesema