Kufuatia ongezeko la uharibifu wa miundombinu ya umeme, vyuma vya barabarani na vya madaraja, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapiga marufuku uuzaji wa vyuma vya shaba (Copper) ambavyo hutumika kujengea miundombinu hiyo.
Hivi karibu Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na maafisa wa Shirika la Umeme [TANESCO] lilifanya operesheni dhidi ya wahalifu na wanaohujumu miundombinu ya umeme ambapo jumla ya watuhumiwa 08 walikamatwa wakiwa na nyaya za umeme pamoja na vifaa mbalimbali kinyume cha sheria.
Aidha katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Idiga hadi Umalila huko Wilaya ya Mbeya walikamatwa watuhumiwa 04 kutokana na kufanya uharibifu na wizi wa miundombinu ya ujenzi wa barabara hiyo vikiwemo vyuma vya barabarani pamoja na nyaya.
Lengo la kupiga marufuku uuzaji wa vyuma vya shaba ni kulinda miundombinu ya Umeme kama vile nyaya za umeme pamoja na miundombinu ya barabara kama vile vyuma vya madaraja na alama za barabarani.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya
SACP – Ulrich Matei