Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Khamis Juma akifungua kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani huko Ukumbi wa Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa makumbusho kutoka Idara ya makumbusho na Mambo ya Kale Bi Kei Mohammed Abdalla akiwasilisha mada ya nguvu ya makumbusho katika Maendeleo endelevu ,wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani huko Ukumbi wa Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Watendaji na Wadau wa Idara ya Makumbusho na mambo yakale wakifuatilia kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani huko Ukumbi wa Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Idara ya makumbusho na mambo ya kale Zanzibar Maryam Mohammed Mansab akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na makumbusho ya Zanzibar wakati wa maadhimisho ya siku ya makumbusho Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini
Mjumbe kutoka Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Salama mohammed akichangia mada ya nguvu ya makumbusho katika Maendeleo endelevu, wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani huko Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Afisa Elimu Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Zanzibar Ramadhan Ali Machano akiwasilisha mada ya nafasi ya makumbusho katika elimu, wakati wa maadhimisho ya siku ya makumbusho Duniani ,huko Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mdau wa mambo ya kale Joshi akichangia mada ya nafasi ya makumbusho katika elimu, wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani, huko Ukumbi wa Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR