MKURUGENZI wa Huduma wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Rajab Moses Mabamba akizungumza leo wakati wa kongamano hilo Jijini Arusha |
Afisa |
MKURUGENZI wa Huduma wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Rajab Moses Mabamba kushoto akiwa kwemye mkutano huo |
NA OSCAR
ASSENGA,ARUSHA
MKURUGENZI
wa Huduma wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Rajab Moses Mabamba amewataka maafisa
rasilimali watu (Maafisa Utumishi) nchini kubadilika na kutumia taaluma zao
kusaidia kuleta matokeo chanya ya taasisi wanazozisimamia na siyo ukwamishaji
Huku
akiwaambia kwamba kazi ya maafisa rasilimali watu ni kusaidia utekelezaji wa
mpango mkakati wa taasisi pamoja na ule wa rasiliamali watu kwa kuwa maafisa
hao ni wadau muhimu kwenye usimamizi wa rasilimali watu na uleta tija .
Rai hiyo
aliitoa leo kwenye Kongamano la kuazimisha siku ya Kimataifa ya Wataalamu wa Rasiliamali Watu na Utawala Duniani ambalo
huazimishwa kila Mei 20 Duniani ambapo kwa hapa nchini linafanyika kwa siku
tatu Jijini Arusha na kushirikisha washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za
Serikali na Binafsi.
Alisema lazima
maafisa rasilimali watu wahakikisha wafanyakazi wanafanya kazi kwa moyo ili
kuwasaidia taasisi kuweza kuleta ufanisi na matokeo chanya kwa kuzingatia
waledi na ubunifu na hivyo kujenga furaha kwa watumishi wanaowasimamia.
“Kongamano
hili ambalo limetuleta pamoja kama maafisa rasilimali watu nchini liwe chachu
ya kwenda kuongeza ufanisi na tija katika maeneo yetu mnayotoka lakini kikubwa
lazima katika utendaji wenu wa kila siku muwe wabunifu kwa lengo la kujenga
uhusiano wa wafanyakazi kufurahia utumishi wao”Alisema Mkurugenzi huyo
Alisema
iwapo wakipata ujuzi wa kuweza kuwasimamia wafanyakazi itawezesha pia kuja na mpango endelevu ambao utawafanya
watumishi kuweza kukaa muda mrefu na hivyo kuweza kulitumikia taifa lao kwa
tija na ufanisi mkubwa utakaochochea kasi ya maendeleo nchini.
“Ujumbe wangu kwenu HCR wote tambueni kuwa
dunia imebadilika na mnatakiwa kusaidia kuleta matokeo chanya ya taasisi na
siyo ukwamishaji wa shughuli za taasisi mnazoongoza”alisema Rajabu.
Awali akizungumza
wakati wa kongamano hilo Afisa Utumishi wa Manispaa ya Temeke Bihagwa Yogwa alisema
mkutano huo umekuwa sehemu nzuri ya kukutana na itawasaidia kuweza kupata
mustakabali kwa namna walivyoweza kuanzisha bodi.
Alisema bodi
hiyo itakuwa inaangalia kwa namna watakavyokuwa wakitekeleza majukumu yao kama maafisa
utumishi,rasilimali watu na kufanya
hivyo kutaongeza mchango wao utoaji huduma kwenye taasisi za serikali na zisizo
za serikali.
Hata hivyo
alisema changamoto wanazokutana nazo inatokana na kutokuwa na chambo kimoja
ambacho kinasimamia mambo yao kwa hiyo kuwa na vyombo kama miavuli vinakuwa vya
shirikisho yanayosimamiwa na watawala na
maafisa rasilimali wao na kuwa na bodi watakuwa na kitu imari na chenye nguvu.
Naye kwa
upande wake Katibu Mkuu wa APAT Christopher
Kabalika aliiiomba Serikali kuona
umuhimu wa kuanzisha bodi ya alisema thibati katika kada hiyo ambayo itakuwa
mwaroibaini wa changamoto zinazowabili.