Wanachama wa WOMESA TANZANIA wakiwa kwenye maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake wanaofanya kazi katika bahari ambapo Tanzania huadhimisha Mwezi Mei 18 kila mwaka. Baadhi ya Mabaharia wakongwe wakiburudika na muziki katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake wanaofanya kazi katika bahari ambapo Tanzania huadhimisha Mwezi Mei 18 kila mwaka.
Baadhi ya wanachama wa WOMESA wakiburudika na Muziki katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake wanaofanya kazi katika bahari ambapo Tanzania huadhimisha Mwezi Mei 18 kila mwaka.
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake wanaofanya kazi katika bahari, Taasisi ya WOMESA TANZANIA wameadhimisha siku hii kwa kufanya matembezi na mazoezi mbalimbali ili kutangaza fursa zilizopo katika sekta ya bahari.
Akizungumza katika maadhimisho hayo leo Mei 18,2022 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Bi.Stella katondo amesema jamii inatakiwa kutambua kuwa kazi za bahari hasa sekta ya usafirishaji zinaweza kufanywa na wanawake kwani sekta hiyo ina fursa nyingi ambazo mwanamke anaweza kuzipata na kuweza kujikimu kiuchumi.
Usafiri baharini umekuwa ukifanywa na wananume kutokana na historia ya kazi yenyewe ilivyo kwamba imekuwa ni kazi ya kuhitaji nguvu na ni kazi ambayo watu wanakwenda mbali na nyumbani kwa muda mrefu.
IMO iliweza kutenga siku moja maalumu kwa kuweza kutambua uwepo wa wanawake lakini vileviile kuweza kuonesha namna gani wanaweza kuwawezesha (traning) ili kuona umuhimu wa kazi hiyo kwa wanawake na kuweza kukubarika.
“Kwakuwa kihistoria kazi hii imekuwa ikifanywa au ikionekana ni kazi ya kufanyika na jinsi ya kiume pia kuna ile hali ya kuona kwamba inakuwaje mwanamke afanye ile kazi na vilevile unakuta kwenye kazi hizi mengi yalishatengenezwa kwamba ni maeneo ya kiume ndo maana unakuta meli nyingi hazitoi hata nafasi ya kuweza kuweka wanawake “. Amesema Bi.Stella Matondo.
Sekta ya Usafiri Baharini inasimamiwa kidunia na Shirika la Bahari Duniani (IMO), kupitia shirika hili liliona ni vyema kuweza kupata nafasi ya kuwanyanyua wanawake hasa kufika katika nafasi za juu za kazi kwenye sekta ya usafirishaji baharini wakaamua kuanzisha Taasisi ya Umoja wa wanawake ambao watakuwa wanasimamia lengo hilo.
Pamoja na hayo Bi.Stella amesema kupitia kuwekwa kwa siku hii muhimu, itavunja vile vikwazo na kuweza kuweka mazingira ambayo yatamuwezesha mwanamke kufanya kazi katika hali ambayo inatakiwa.
Kwa upande wake Katibu wa Taasisi ya WOMESA TANZANIA Bi.Devota Mandanda amesema katika maadimisho hayo wamewashirikisha mabaharia wakongwe, wanafunzi kutoka shule mbalimbali na wadau wengine wa sekta ya bahari ili kuona ni namna gani jamii ikafahamu yakuwa kazi za bahari hata wanawake wanaweza.
Amesema wameamua kuwashirikisha wanafunzi maana kuna wanafunzi wana ndoto za kufanya kazi katika bahari hivyo kupitia siku hii watafahamu fursa zilizopo katika sekta hii na kutamani kufanya kazi hii.