****************
KATIKA wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara ya kukagua maeneo yote yaliyofanyiwa ukarabati katika majengo ya Hospitali ya Tumaini wilayani Hangan mkoan Manyara huku akitumia nafasi hiyo kushirikiana na wananchi kwa vitendo kwa kuamua kupanda juu ya paa kupaka rangi.
Akizungumza baada ya kukagua majengo ya hospitali hiyo na kisha kushiriki kupaka rangi ya moja ya paa lililopo kwenye hospitali hiyo, Shaka ameonesha kuridhishwa na kasi ya ukarabati huo uliofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo.
“Tunawapongeza viongozi wa Wilaya na wananchi wote kwa kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za maendeleo.Nimeridhishwa na ukarabati unaondelea kwenye hospitali hii, rai yangu hakikishe mnakamilisha haraka ili wananchi waendelee kupata huduma za matibabu ya afya,”amesema Shaka huku akiwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali.
Katika taarifa iliyosomwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia ametoa Sh.milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya ambalo ujenzi wake bado unaendelea na utakamilika kwa wakati.“Tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Rais tunampongeza kwa uamuzi wake wa kutoa fedha kwa ajili ya hospitali yetu.Tunasema ahsante.”