******************
Adeladius Makwega-TANGA
Haiba ni muonekano wa mtu namna alivyo, haiba pia ni mojawapo la somo kubwa sana kwa wakurufunzi. Wakitajiwa aina mbili za haiba nazo ni ya ndani na ya nje.
Wanafunzi wa Ualimu (Wakurufunzi) wanasisitizwa kuwa na haiba nzuri ya ndani na ya nje. Aina zote hizo za haiba zina umuhimu mkubwa kwa mwalimu kukamilisha jukumu lake la kuwasomeshwa wanafunzi wake.
Haiba Nzuri ya Ndani inamjenga mwalimu kutenda haki bini haki kwa wanafunzi wake, mathalani kutoa ushauri mwema na hata kutoa alama za masomo kwa haki.Huku tabia hizo zikiwapa nafasi wanafunzi kuiga yaliyo mema.
Haiba ya Nzuri Nje, hii inatoa nafasi ya wananafunzi kutokupeleka mawazo yake katika mambo mengine na kutilia mkazo katika kile anachafundishwa tu, haiba hii pia inaweza kuigwa na mwanafunzi nayeye kuwa na haiba nzuri.
Msomaji wangu pata picha ya mwalimu anayevalia nguo za kubana zinazoonesha maungu yakeya ndani alafu ameingia darasani kusomesha somo lake jambo hilo linaweza kuwafanya wanafunzi kutokutilia maanani somo hili kabisa. Lakini pia haiba hiyo mbaya inaweza kuigwa na wanafunzi hao na kuikengeusha jamii yetu.
Mwanakwetu kuna aina nyingine ya mwalimu ambayo ni viongozi wetu. Hali inakuwa ya nafuu kwa mwalimu wa darasani kwa kuwa yeye anaonekana na watu wachache lakini viongozi wanaonekana na hadhira kubwa mno.
Kwa viongozi ni muhimu mno kuwa na haiba nzuri kwani huigwa mambo yao kwa haraka ikiwamo mavazi. Japokuwa inawezekana kiongozi akawa na mapenzi na mavazi fulani kuyavaa anaweza kuyavaa akiwa katika mazingira binafsi na siyo ya hadhara ambayo ni mazingira ya jamii.
Pengine kiongozi amesimama jukwaani anasisitiza kilimo, watu badala ya kusikiliza juu ya kilimo wanatazama namna alivyovaa kiongozi wao na wakiulizana kuwa mtindo huu unapatikana wapi?
Ndiyo kusema darasa la viongozi lina wanafunzi wengi sana kwa hiyo wanatakiwa kuwa na haiba madhubuti maradufu.
Mwalimu Julius Nyerere akiwa Rais Tanzania alitengeza haiba ya uvaaji wa suti zisizo na kola–CHUU LAI kwa hiyo hata alipokuwa akifanya ziara jamii inatambua kuwa Nyerere wa picha katika magazeti ndiyo alivyo hata ukikutana naye moja kwa moja jamii inamgoja kumsikia anasema nini? Maana ajenda ni maendeleo na siyo kukogana kimavazi. Huku dhana ya kushiriki katika kukogana ni walimbwende peke yao.
Kati ya mwaka 2016-2022 nimekuwa nikivutiwa na haiba madhubuti maradufu ya INJINIA ZENA AHMED SAID ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mwanakwetu ufuatiliaji huo wa miaka kati ya moja na saba umekuwa wa karibu na mbali na nimebaini kuwa haiba ya kiongozi huyu ni nzuri na imekuwa haibadiliki huku ikivutia mno jamii anayoiongoza kuwekeza mawazo yao kwa kile anachokielekeza na siyo mavazi yake. Siyo sijui leo atavaaje? Bali leo atatoa maagizo gani?
Injini Zena huvaa nguo ndefu, zinazomkaa vizuri sana na kuwa huru kusongelea meza kuu au marufaa na hata kuitazama hadhira yake bila shaka yoyote. Kichwa chake hufungwa kilemba kwa rangi haipendayo lakini mara nyingi isiyowaka sana. Macho yake uongozewa nakshi na miwani mikubwa miyeupe.
Mavazi hayo yamekuwa yakimpendeza mno na kusaidia kumuonesha anayetazama kuwa ni huyo huyo ambaye anayemuona kila siku.
Nguo zake ndefu hizo zilizoifunika sakafu hupambwa na sauti ya hatua za viatu vyake vinavyatamba katika sakafu au malumalu anayoikanyaga.
Mambo unoga zaidi hasa hasa pale anapomalizia na tabasamu maridhawa linalosaidia kuyafikisha vizuri maelekezo ya serikali kwa walengwa, maelekezo yawe ya miradi ya maendeleo au kwa watumishi wa umma
Mwanakwetu nani alikwambia wananchi tunapenda maelekezo ya serikali yetu yatolewa na watu waliokunja sura? Hakika Injinia Zena na haiba mara dufu.