*********************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya yanga leo imelazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya Ruvu Shooting mchezo uliopigwa katika dimba la Lake Tanganyika Mkoani Kigoma, mchezo ambao Ruvu Shooting alikuwa mwenyeji.
Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya aina yake licha ya Mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Mayele kugongesha mwamba mara mbili hakuweza kufunga kabisa kwenye mchezo huo ambao unakuwa wa pili kutokufunga mara baada ya kushindwa kutikisa nyavu kwenye mchezo uliopita.
Yanga inaendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu NBC licha ya matokeo hayo ya sare na Simba Sc anabaki nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 13.