WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB),Prof. Hamisi Dihenga lleo April 30,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati alipokutana na Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) leo April 30,2022 jijini Dodoma.Kushoto ni Katibu Mkuu wake Prof. Eliamani Sedoyeka
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akifafanua jambo wakati akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) leo April 30,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka (katikati) wakati wa mkutano na Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) leo April 30,2022 jijini Dodoma.kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB),Prof. Hamisi Dihenga,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,mara baada ya kukutana na kuzungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) leo April 30,2022 jijini Dodoma
Mwandishi wa habari kutoka Muungwana blog Ezekiel Mtonyole akimuuliza swali Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) leo April 30,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa kikao na Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) leo April 30,2022 jijini Dodoma.
………………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, amesema kwa mwaka wa fedha ujao wa 2023/24, Serikali inatarajia kupanua wigo wa utoaji mikopo kwa elimu ya ufundi ngazi ya Stashahada hususan kwa ujuzi na ufundi unaohitajika kwenye soko la ajira.
Hayo ameyasema leo April 30,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB), Prof,Mkenda amesema kuwa kuna umuhimu wa kupeleka mikopo katika elimu ya ufundi walau ngazi ya Stashahada(Diploma) kwenye vyuo vya ufundi.
Prof,Mkenda ameitaka Bodi hiyo kujipanga ili ifikapo mwaka wa fedha 2023/24 kuanza kutoa mikopo kwa wanafunzi watakaosoma masomo ya Ufundi na ujuzi kwa ngazi ya Diploma.
“Kilio cha watu wengi kwasasa ni ajira, sasa sehemu ambayo ajira ni rahisi zaidi ni kwenye ujuzi na ufundi, kwa hiyo vyuo kama DIT, Arusha Technical, tumekubaliana kazi ifanyike tuone mwaka mpya wa fedha, ukiacha mwaka huu tuwe tumejiandaa kupeleka fedha kwa ajili ya ufundi, tungependa tuseme mapema ili watakaotaka kuomba sehemu ya kusoma watambue sehemu hii sasa itakuwa na fursa ya kupata mikopo.” amesema Prof. Mkenda.
Kuhusu kutoa ufadhili kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi, Prof.Mkenda amesema kuwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara imetenga fedha kwa ajili ya kutoa ufadhili wa elimu ya juu (scholarships) kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
Prof.Mkenda amesema kuwa ufadhili huo utatolewa kwa asilimia mia moja kwa wanafunzi wachache na watasomeshwa ndani na nje ya nchi.
Amesema lengo la Serikali ni kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya juu na kuhamasisha watoto wengi kupenda kusoma masomo ya Sayansi.
Mhe. Mkenda ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka bilioni 464 hadi kufikia bilioni 570, kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya wanaochelewa kurejesha mikopo na kufuta asilimia 6 ya kulinda thamani.
Aidha Waziri Mkenda ametoa wito kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu juu kutoa taarifa zote zinazotakiwa kwa ukamilifu na kwa wakati ili waweze kupata mikopo hiyo bila changamoto.
“Mkopo unatolewa kulingana na taarifa anazotoa mwombaji, ukitoa taarifa ambazo sio kamili kunakuwa na changamoto hivyo toeni taarifa kamili na Bodi itaendelea kuchakata taarifa hizo ili wanaostahili kupata mikopo wapate,” amefafanua Prof. Mkenda.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka amesema kwa sasa Wizara imejipanga kuhakikisha Watanzania wengi wanapata fursa ya kusoma elimu ya juu kwa kuwezesha kufanya hivyo kulingana na malengo ya Taifa letu.
“Wote tunafahamu juhudi ambazo Serikali imeweka kwenye elimu msingi ambazo zimepelekea kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na sita na wakiwa na ubora na kupelekea kuwa na vigezo vya kuendelea na elimu katika ngazi inayofuata hivyo kupekelea kuhitajika fedha kwa ajili ya kusomesha,” amesema Prof. Sedoyeka.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB),Prof. Hamisi Dihenga amesema anatambua kuwa wana dhamana kubwa ya kuhakikisha utaratibu wa kutoa mikopo unaeleweka kwa Watanzania wote na unawasaidia wale wanaostahili kupata mikopo.