Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Japhet
Kashaigili akifafanua jambo wakati wautoajiwa uwasilishwaji wa matoke ya utafiti wa miaka mitano wa chanzo cha maji cha Jiji la Dodoma Makutupora.
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji
kutokaWizaraya Maji Dkt George
Lugomela akitoa neno wakati akifungua Warsha hiyo ya siku moja ya kupokea matokeo ya utafiti wa mradi wa GroFutures Jijini
Dodoma.
Tayrol kutoka katika Chuo Kikuu cha jiji la London
nchini Uingereza akichangia kwenye uwasilishaji wa matokeo hayo.
1Mmoja ya wakulima ambao wamepata nafasi ya kuhudhuria Warsha hiyo kwa niaba ya wa kulima wengine Dkt.
Huruma Msuya akizungumza na SUA MEDIA nje ya Warsha hiyo.
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff
cha nchiniUingereza Dkt. Adrian Healy akizungumza wakati akiwasilisha sehemu ya utafiti wake.
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi,
Watafiti pamoja na wadau wengine kutoka sekta mbalimbali walioshiriki katika warsha hiyo ya kutoa matokeo ya utafiti
huo.
1. Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini
Dodoma.
Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Amina Hezron na Calvin Gwabara, Dodoma.
MATOKEO ya Utafiti yanaonyesha kuwa shughuri za kibinadamu
zinazofanyika katika maeneo ya dakio bonde la maji chini ya ardhi la makutupola
ambalo ndio chanzo kikuu cha maji cha Jiji la Dodoma zinauwezekano mkubwa wa
kuathiri uwepo wa chanzo hicho cha maji endapo jitihada za makusudi
hazitachukuliwa kulinda chanzo hicho.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mtafiti kutoka katika Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Japhet Kashaigili katika warsha ya
mawasilisho ya matokeo ya Utafiti ulioangalia maji chini ya ardhi katika ukanda
wa kusini mwa la Sahara mbele ya wadau wa chanzo hicho cha maji uliofanywa na
Watafiti wa SUA kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Cardiff na Chuo Kikuu cha
Jiji la London Uingereza.
Prof.Kashagili amesema kuwa bila kukaa kwa pamoja kujadiliana
namna bora za kulinda eneo hilo sasa chini ya mpango wa upangaji wa Makazi,
athari yake itakuwa kubwa ambayo itapelekea kulipa pesa nyingi huko baadae.
“Kuna haja ya kuyaangalia haya mapema ikiwezekana bonde hili
litangazwe lote kwenye Gazeti la Serikali kuwa sehemu ya hifadhi ya bonde na
liangaliwe kwa upekee wake ili kuzuia shughuri za kibinadamu ambazo zinaweza
zikaathiri eneo lile kutokana na umuhimu wake kwakuwa kimsingi ukiangalia
tathimini ya maji mbalimbali ambayo yametokana na vyanzo mbalimbali
karibuni zaidi ya asilimia 90 za maji ya mji huu wa Doodoma yanatoka pale
”, ameeleza Profesa Kashaigili.
Aidha Prof Kashaigili ameongeza kuwa kwakuwa mvua kwa miaka ya
karibuni hazijawa kuwa kufikia zile za El nino zinaweza tumiaka mbinu zingine
ambazo zimetumiwa nan chi zingine duniani za kuchimba visima na kuruhusu maji
kujaa kwenye eneo hilo na kuyaacha yaingie kwenye mwamba huo ardhini na kisha
kuweza kuyatumia kupelekwa kwenye maeneo mengi zaidi ya jiji la Dodoma.
“Inawezekana haya maji tukayatathimini ubora wake lakini
tukayaruhusu yakakaa juu ya ardhi kwakuweka mazuio mbalimbali ili yaweze
kunywea kuingia ardhini jambo ambalo nchi mbalimbali zimefanya hivyo na
zimefanikiwa kuondoka na adha zilizopo za upatikanaji wa maji”, alifafanua
Profesa Kashaigili.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya
Maji Dkt George Lugomela ameeleza kuwa kwa siku jijini Dodoma linahitajika mita
za ujazo 133,845 upatikananji wake ni mita za ujazo 66,600 kwa siku ambayo ni
kama nusu ya mahitaji na hii ni kutoka na ongezeko la watu katika jiji hilo.
“Serikali tayari imeweka mikakati Madhubuti katika kuhakikisha
changamoto hii inatatuliwa ikiwemo kuchujenga bwawa la FAKWA lakini mkakati wa haraka
ni kuchukua maji mita za ujazo 100,000 kwa siku kutoka bwawa la Mtera ambazo
ukichanganya na zile 66,600 za sasa unapata mita za ujazo 166,600 ambazo
zitakuwa na uwezo wa kukidhi kabisa mahitaji ya Jiji lote la Dodoma” alifafanua
Dkt. Lugomela.
Hivyo amesema kuwa matokeo ya Utafiti huo ni muhimu sana na
yatatumiwa na Wizara katika kuwezesha kutazama namna ambavyo itawezekana
kutatua changamoto hiyo ya maji kupitia chanzo cha Makutupola tofauti na ilivyo
hivi sasa.
Nae Mtafiti Mkuu wa mradi huo Profesa. Richard Tayrol kutoka
katika Chuo Kikuu cha jiji la London nchini Uingereza amesema kuwa mradi huo
unatekelezwa katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Nigeria na Ethiopia pamoja na
malengo mengine lakini pia unalenga kuangalia namna maji yaliyo chini ya ardhi
yanavyoweza kuchangia katika kuondoa umasikini.
Ameeleza kuwa maji ya chini ya ardhi hayawekewi mkazo sana kama
ilivyo kwa maji ya juu ya ardhi hivyo ameishauri Serikali kuwekeza katika maji
yanayopatikana chini ya ardhi kakuwa kuna maji mengi kuliko haya tunayoyaona
juu ya ardhi yanayopita kwenye mito na maziwa.
“Naishauri Serikali kuwekeza nguvu, muda pamoja na kuwajengea
uwezo watu wake katika kutambua rasilimali hii ya maji yaliyopo chini ya ardhi
maana katika fani ya hydrolojia, kwani itasaidia katika kukabiliana hata na
mabadiliko ya tabia nchi na kuchangia katika matumizi mbalimbali kama vile
Kilimo,Viwanda na matumizi ya nyumbani ”, alisema Profesa. Tayrol.
Naye mmoja ya wakulima ambao wamepata nafasi ya kuhudhuria Warsha
hiyo kwa niaba ya wakulima wengine Dkt. Huruma Msuya ameishauri Serikali
kutenga maeneo maalumu kwaajili ya misitu kilimo cha mbogamboga na matunda
kwaajili ya kulisha miji jambo litakalosaidia mji kuwa na sehemu ya
kupumulia.
“Tusifanye makosa kama yaliyofanyika kwenye Jiji la Dar Es
Salaam ambapo mji umekuwa tu kutoka Kariakoo mpaka Kibaha bila kuwa na
maeneo yenye mashamba na Misitu, mji usikue tu kuwe na miji midogo midogo
pembeni ya mji mkubwa ambayo nayo itakuwa imeendelea itakuwa inapata maji
hukohuku kupunguza hali ya upatikanaji wa maji kutoka upande mmoja”, alisema
Dkt Msuya.
Matokeo ya tafiti yaliyowasilishwa ni matokeo ya Uafiti
iliyofanyika kwa miaka mitano na mradi wa GroFutures ulioanzishwa na Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Chuo cha Cardiff kilichopo nchini
Uingereza pamoja na Chuo Kikuu cha jiji la London nchini Uingereza .