Afisa kutoka Idara ya Maendeleo na Vijana iliyopo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sheila Makungu Mwinyi akitoa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST), Kuhusu kutumia Fursa mbali mbali zinazotolewa kwa Vijana ikiwemo Mikopo, kwa lengo la kujiajiri, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt. Idrissa Muslim Hija. Mbweni Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST) Dkt. Mahmoud Abdulwahab akitoa neno la shukurani kwa Wanafunzi wa Chuo cha AP kutoka Belgum, wakati akiwaaga mara baada ya kufanya Project mbali mbali kwa Muda wa Mwezi Mmoja, kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST), hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Idrissa Muslim Hija, Mbweni Mjini Zanzibar.
PICHA NA MARYAM KIDIKO – KIST.