Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akionesha namna kifaa cha upimaji ardhi kijulikanacho kama Total Station kinavyofanya kazi mara baada ya kufika katika banda la maonesho la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi yanayoendelea jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akielekezwa namna kifaa cha upimaji ardhi kijulikanacho kama Total Station kinavyofanya kazi na Bi. Fatuma Hamisi ambaye ni mpima ardhi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kufika katika banda la maonesho la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi yanayoendelea jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akitia sahihi kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika banda la maonesho la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi yanayoendelea jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kufika katika banda la maonesho la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi yanayoendelea jijini Dodoma
…………………………………………………….
Na Anton Ishengoma
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi wakati zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakapoanza ili kutoa taarifa zitakazowezesha Serikali kupanga mipango bora ya maendeleo ya ardhi ikiwemo mipango miji lakini pia suala zima la maendeleo ya watu.
Wizara ya Ardhi itatumia Sensa ya Watu na Makazi kufanya zoezi la sensa ya Makazi nchini ili kuiwezesha wizara hiyo kubaini makazi yaliyopo ikiwemo ambayo bado yanaendelezwa ili iweze Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi ikiwemo suala zima la mipango miji.
Naibu Waziri Kikwete alitoa rai hiyo jana alipofika katika Maonesho ya Wiki ya Afya ya na Usalama mahali pa kazi katika maeneo ya kazi ambayo kilele chake ni Siku ya Kazi Duniani maarufu Mei Mosi yanayoendelea jijini Dodoma na kutumia fursa hiyo kuwataka watanzania kushiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
‘’Kwasisi kupata taarifa za kina juu ya watu na makazi hapa Nchini pamoja na taarifa nyingine za kina itatusaidia kupanga mipango miji lakini kupanga maendeleo ya watu na namna bora yakufanikisha maendeleo endelevu kwa kipindi cha miaka mia moja ijayo.’’Aliongeza Naibu Waziri Kikwete.
Aidha Kikwete aliongeza kuwa dodoso la Sensa lina maswali mengi lakini sio tu tutaangalia nyumba zilizo tayari lakini pia zile ambazo ziko katika hatua ya awali ya ujenzi kama msingi kwani nazo zitaendelezwa na kuwa nyumba kamili.
Kikwete aliongeza kuwa pamoja na kutambua makazi lakini pia wataangazia suala la maeneo yaliyotengwa ikiwemo makaburi,viwanja vya biashara na makazi ili kuiwezesha Wizara ya Ardhi kupanga shughuli za kimaendeleo katika nchi yetu.
Aidha Kikwete aliongeza kuwa ushiriki wa Wizara katika Maonesho haya nikuwaonesha watanzania juu ya mambo makubwa yanayotekelezwa na Wizara ya Ardhi katika kipindi cha uongozi wa awamu ya sita.
Kikwete alisisitiza umuhimu wa wananchi kufika katika maonesho haya ili waweze kujionea ubunifu wa wafanyakazi katika kutumikia wananchi lakini pia kubaini yale ambayo serikali yao inafanya ili kuwaletea maendeleo.
Naye Mbunge wa jimbo la Hanang Muhandisi Samweli Kayunga aliongeza kuwa amepata elimu ya kutosha kuhusu mabaraza ya ardhi baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kujionea na kupata elimu ya masuala ya ardhi.
Maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama mahali pakazi yanendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre na Kilelele chake itakuwa ni Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi Mei Mosi.