MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 58 YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAREHE 26 APRILI, 2022
Tarehe 26 Aprili, 2022 tutaadhimisha Miaka 58 ya Muungano wa Tanzania. Hili ni tukio muhimu na la kihistoria kwa Taifa letu. Katika maadhimisho hayo, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa 3,826.
- 2.
Kwa masharti yafuatayo:
(i)
Wafungwa wote wapunguziwe robo (1/4) ya vifungo vyao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu cha 49 (1) cha Sheria ya Magereza, Sura ya 58. Wafungwa hao sharti wawe wametumikia robo (1/4) ya vifungo vyao na wawe wameingia gerezani kabla ya tarehe 26 Februari, 2022 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika sharti la 2(i–ii);
(ii) Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu ambao wametumikia
robo (1/4) ya vifungo vyao na wapo kwenye Terminal Stage, ugonjwa huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya;
(iii) Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi ambao
wametumikia robo (14) ya vifungo vyao. Umri huo uthibitishwe na jopo la
waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya;
(iv) Wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa na watoto wanaonyonya,
wasionyonya na wajawazito ambao wametumikia robo (1/4) ya vifungo
vyao; (V) Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (physical disability and
mental disability) ambao wametumikia robo (1/4) ya vifungo vyao. Ulemavu huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya;
(vi) Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kuwekwa kizuizini (Under
President’s Pleasure) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea;
(vii) Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo ambao wamekaa gerezani
kuanzia miaka thelathini (30) na kuendelea;
(viii) Wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha gerezani ambao wamekaa
gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea;
(ix) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya kujaribu kuua (Attempt
to Murder) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea;
(x) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya kujaribu kujiua
(Attempt Suicide) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na
kuendelea;
(xi) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya kuua watoto wachanga
(Infanticide) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi na tano (15) na kuendelea;
(xii) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya uhujumu uchumi
ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea;
(xiii) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya matumizi mabaya ya
madaraka yao ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka mitano (05) na
kuendelea;
(xiv) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya utakatishaji wa fedha
ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea;
(xv) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya rushwa ambao
wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea;
(xvi) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya usafirishaji wa madawa
ya kulevya ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea;
(xvii) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya utekaji au wizi wa
watoto ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea; na
(xviii) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya wizi au ubadhirifu wa
fedha na mali za umma ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi na tano (15) na kuendelea.
- 3.
Aidha, msamaha huu usiwahusishe wafungwa wafuatao:
(i)
(ii)
Wafungwa wa madeni; na Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi za Parole, Sura ya 400 Sheria ya Huduma kwa Jamii (Sura ya 291) na Kanuni za Kifungo cha Nje {The Prisons (Extra Mural Penal Employment) Regulations}, 1968.