*******************
CHAMA cha Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam, wamekanusha taarifa iliyosmabaa mtandaoni iliyotolewa na Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania kuhusu kutokushiriki kwa wamachinga kwenye Maonesho ya Biashara yanayotarajia kufanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam Bw.Namoto Yusuph amesema wamesikitishwa na taarifa hiyo ambayo ilisema mwaka huu hakutakuwa na ushiriki wa machinga kwenye maonyesho ya Biashara ya kimataifa Dar es salaam na kama kuna mtu atahitaji kushiriki basi atahitajika kulipia shilingi milioni moja kama taasisi nyingine.
Amesema kuwa taarifa hiyo imeleta taharuki kwa wananchi walio wengi hivyo taarifa kama hiyo ingetakiwa itolewe na Mamlaka ya Biashara TAN TRADE.
“Niseme kuwa sisi kama wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam tulishiriki mwaka jana katika maonyesho tulikipia kiingilio cha laki moja na tukapewa meza kiti na kitambulisho hivyo taarifa hizo zilizosambaa siyo za ukweli zipuuzwe kiingilio hakijapanda kufikia kiasi hicho”alisema Namoto
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Wamachanga Mkoa wa Dar es salaam Bw.Masoudy Chauka ametoa taarifa kwa viongozi wote wa wamachinga kuwepo kwa mfumo data wa machinga Pamoja na mfumo wa sacos ilikuwatambua wamachinga wote na kutatua changamoto zinazo wakabili.