Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Eric Hamiss (kushoto) akifafanua jambo kwa viongozi wa CCM wakiwemo watumishi wa kampuni hiyo kabla ya uongozi huo wa Chama kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa meli na ukabati wa meli za MV. Butiamana MV. Victoria kwenye bandari ya Mwanza Kusini.
Meneja wa mradi wa ukabarati wa meli na ujenzi wa meli mpya,Meja, Mhandisi Abel Gwanafyo (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa uongozi wa CCM ulipokwenda kukagua miradi hiyo jana kwenye Bandari ya Mwanza Kusini.Kulia ni Mkujumbe wa NEC, Jamala Abdul Babu, wa pili ni Mwenyekiti wa Mkoa Dk. Anthony Diallo na wa tatu kutoka kushoto ni Katibu wa mkoa, Salum Kalli, aliyeinama ni Mtendaji Mkuu wa MSCL, Eric Hamis.
Ujumbe wa CCM Mkoa wa Mwanza ukiongozwa na meneja wa mradi wa ujenzi na ukarabati wa meli, Mhandisi Meja Abel Gwanafyo (wa kwanza kushoto) kukagua eneo linalojengwa chelezo ya meli mpya jana.Wa pili ni Mtendaji wa MSCL Eric Hamiss,wa tatu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Dk. Anthony Diallo.Kutoka kulia wa pili ni Katibu wa mkoa Salum Kalli na wa tatu ni Mjumbe wa NEC, Jamal Abdul Babu.
Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza, wakipata maelezo mafupi ya mradi wa ukarabati wa meli za MV. Victoria na MV. Butiama kutoka kwa Mhandisi Abel Gwanfyo (wa tatu kutoka kulia) jana kabla ya kukagua ukarabati huo wa meli.Kulia ni Katibu wa Mkoa Salum Kalli, wa pili ni mwenyekiti wa mkoa, Dk. Anthony Diallo.
Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Dk. anthony Diallo na Salum Kalli, wakiiingia ndani ya meli ya MV. Victoria inayokarabatiwa kwa gharfama ya sh bilioni 22 na kampuni ya Korea Kusini ya KMTI.
Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza wakiangalia mafundi (hawapo pichani) wakikata vyuma vinavyotumika kwenye ukarabati wa meli ya MV. Victoria jana. Mbele ni Mwenyekiti wa CCM Dk. Anthony Diallo na kulia ni Katibu Salum Kalli.
Mhandi wa MSCL Meja mstaafu Abel Gwanafyo, akiwapa maelezo ya mradi wa ukarabati wa meli ya MV. Victoria , viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo (kushoto) na Katibu wa mkoa Salum Kalli wakishuka kutoka kwenye meli y MV. Victoria baada ya kukagua na kujionea shughuli za ukarabati wa meli hiuo.Kushoto chini ni Mhandisi, Meja Abel Gwanfyo ambaye ni meneja wa mradi huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza. Salum Kalli akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuhimisha ziara ya ukaguzi wa mradi wa ukarabati wa meli na ujenzi wa meli mpya.
picha zote na Baltazar Mashaka