wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na kamati hiyo wakikagua ujenzi wa barabara ya Mtwira Darajani Ikonongo ya
kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami
kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa.
Mjumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ambaye ni afisa wa TAKUKURU wilaya ya Iringa Anneth Mwakatobe akishirki katika zoezi la ukaguzi wa barabara ya Mtwira Darajani Ikonongo ya
kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya
wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na kamati hiyo wakikagua ujenzi wa barabara ya Mtwira Darajani Ikonongo ya
kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami
wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na kamati hiyo wakikagua ujenzi wa barabara ya Mtwira Darajani Ikonongo ya
kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami.
Na Fredy
Mgunda,Iringa
KAMATI
ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa imeridhishwa na utendaji wa kazi wa
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) baada ya kukagua ujenzi
wa barabara ambazo wanazisimamia katika manispaa ya Iringa.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukagua miradi,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya
wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema
kuwa TARURA wamekuwa wakifanya kazi nzuri za kusimamia miradi ya ujenzi wa
barabara kulingana na thamani ya fedha ambazo zimetolewa na serikali.
Moyo
alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Mtwira Darajani Ikonongo ya
kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami kutasaidia kuchochea uchumi wa wananchi kwa
kufanya shughuli zao kwa haraka Zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.
Alisema
kuwa wilaya ya Iringa inamtandao wa barabara zinazotambulika zenye jumla ya
kilometa 2173.44 ikiwa kilometa 1631.67 katika halmashauri ya wilaya ya Iringa
na kilometa 541.77zipo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa zote zipo chini
ya TARURA.
Moyo alisema
kuwa barabra hizo zote zinahudumia wananchi wa maeneo mbalimbali katika usafiri
na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali za uchumi ambazo zote hizo husaidia kukuza
maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Iringa kwa ujumla.
Alisema
kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa imeridhishwa na
utekelezwaji wa ujenzi wa barabara zilizopo chini ya TARURA na kuwata wataalam
kuendelea kuwasimamia hivyo hivyo wakandarasi ambao wamepewa tenda ili
watekeleze ujenzi kulingana na thamani ya fedha ambayo inakuwa imetolewa.
Wakati
wa ziara hiyo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ilimpongeza
meneja wa TARURA wilaya ya Iringa Eng Barnabas Jabiry kwa kazi kubwa
anayoifanya ya kusimamia vilivyo miradi ya ujenzi wa barabara ambazo
wanazisimamia katika wilaya ya Iringa.
Awali
meneja wa TARURA wilaya ya Iringa Eng Barnabas Jabiry alisema kuwa ujenzi wa
barabra ya Mtwira Darajani Ikonongo ya kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami
utagharimu kiasi cha shilingi 500,000,000 hadi kukamilika.
Eng Jabiry
alisema kuwa mradi huo ukikamilika utapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa
kata za Mkwawa,Mtwivila na Kihesa kwa kuwa itakuwa inapitia vizuri bila
usumbufu wowote ule na kuwasaidia wananchi kufanya shughuli za uchumi bila
usumbufu wowote ule.
Alisema kuwa
mradi huoumeweza kutoa ajira 76 kati ya hao wanawake 10 wanaume 66 ambao wote
wanapatikana katika kata hiyo na maeneo ambayo yanaizunguka kata hiyo
Eng Jabiry
alisema kuwa anaishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuwezesha ukarabati za vijijini na mjini pamoja na madaraja ili kurahisisha
usafiri nauchukuzi kwa kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabra kutoka shilingi
bilioni 1.46 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na kufikia shilingi bilioni 2.46 kwa
mwaka wa fedha wa 2021/2022 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia Zaidi ya 68.