Timu ya wanawake ya Uchukuzi SC (Kulia) wakiwavuta Wizara ya Afya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa 2-0 katika mchezo wa kuvuta kamba katika michuano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Timu za wanaume ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) (kushoto) wakivutwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa 2-0 michuano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1
Timu ya wanawake Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) (kulia) wakiwavuta Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa mivuto 2-0 kamba wa michuano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1
Wachezaji wa timu ya wanaume ya Wizara ya Mambo ya Ndani (Kulia) wakijaribu kuzuia kuvutwa na Uchukuzi SC, hatahivyo wamevutwa kwa mivuto 2-0 katika michuano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Goli kipa Diana Kami (watatu kutoka kushoto) wa timu ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) akijaribu kuuwahi mpira mbele ya Irene Batanyita wa Uchukuzi SC walipochuana katika mchezo wa netioboli wa kuwania kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo Uchukuzi wameshinda kwa kishindo kwa magoli 52-1.
Kipa Emmanuel Boniface wa timu ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) akijaribu kumzuia mshambulaiji Sauli Malamla (mwenye mpira) wa timu ya Ukaguzi, ili asilete madhara kwenye lango lake. Katikati ni Lameck Lima wa TRA. Timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2 katika michuano ya kombe la Mei Mosi Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma..
…………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) zimefanya mauaji kwa kuwafuinga wapinzani wao katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali jijini Dodoma.
Mambo ya Ndani wamewafunga Mamlaka ya Mapato nchini (TRA kwa kuwafunga magoli 79-8, hadi mapumziko washindi walikuwa mbele kwa magoli 41-6; nao Uchukuzi waliwachapa ndugu zao wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa magoli 52-1 washindi waliongoza kipindi cha kwanza wakiwa na magoli 25-0.
Katika mechi nyingine za netiboli timu ya Wizara ya Kilimo waliwachapa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa magoli 26-13; nayo Benjamin Mkapa Hospital waliwafunga Wizara ya Maji kwa magoli 23-21; huku Mzinga wakizinduka kwa kuwafunga Wizara ya Madini kwa 27-10. Mamlaka ya Mapato nchimi (TRA) wamewafunga Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini kwa magoli 28-16;
Halikadhalika nao Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wamechapwa na Mfuko owa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa magoli 31-16; huku Kongwa DC wakitoka sare na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa magoli 14-14.
Katika michezo ya soka uliofanyika kwenye uwanja wa Shell Complex (Wajenzi), timu ya Uchukuzi SC waliwafunga Wakala wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwa bao 1-0, lililofungwa na Lugano Mwasomola; huku timu ya Manispaa ya Temeke waliwachapa Wizara ya Afya kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Sunday Mwakijale na Masoud Masoud; nayo TRA walitoka sare na Ukaguzi kwa 2-2.
Michezo mingine na matokeo yakiwa kwenye mabano timu ya Hazina ilitoka sare na Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) kwa (2-2); huku Benjamin Mkapa Hospital (1) vs Wizara ya Nishati (2); Ulinzi (1) vs Wizara ya Maji (0); Chuo Kikuu cha Dodoma (2) vs Wizara ya Maliasili na Utalii (3); na NSSF (1) vs TARURA (1); UDOM tena wametoka sare na Wizara ya Maji kwa 2-2..
Kwa upande wa wanawake timu ya Uchukuzi SC waliwavuta Wizara ya Afya kwa 2-0; huku NEC wakivutwa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa 2-0; nao Mahakama waliwavuta TANESCO kwa 2-0; Wizara ya Utamaduni, Sanaa na michezo wamevutwa na Hazina kwa 2-0; TAMISEMI (1) TANROADS (0); NCAA (2) vs Wizara ya Mambo ya Ndani (0); TPDC (2) vs Ofisi y Waziri Mkuu (0); nayo Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (2) vs Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (0); Wizara ya Maji (2) v Ofisi ya Waziri Mkuu (0) na Uchukuzi SC (2) vs Chuo cha Mipango (0).
Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume timu ya Uchukuzi waliwachezesha kwata Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kuwavuta mivuto 2-0; huku TPDC (2) vs Shirika la Umeme nchini (TANESCO) (0); NEC (2) vs TARURA (0); Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (0) vs Hazina (2); Wizara ya Maliasili na Utalii (0) vs Chuo cha Mipango (2); huku timu zilizopata ushindi wa chee baada ya wapinzani wao kuingia mitini ni pamoja na Wizara ya Kilimo baada ya Ukaguzi kuingia mitini; na NCAA baada ya Wizara ya Maji kutoonekana kiwanjani.
Nayo Kamati ya mashindano hayo imesema imeridhishwa na kiwango kinachooneshwa na wachezaji wa michezo mbalimbali ambao wanaonesha mchezo mzuri na kutoa burudani kwa mashabiki
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Hamis Mkanachi amesema tangu kuanza kwa michuano hii tarehe 16 April, 2022 hadi sasa timu zote 41 zinazoshiriki michezo hiyo zimeonesha viwango vya juu, ambapo kaulimbiu ya michezo hiyo ni “Michezo ni Afya na huamsha ari ya Kazi, Cheza, Chanja na Jiandae kuhesabiwa kwa Maendeleo ya nchi”