Mchezaji Devota Kaguta (WA) wa timu ya Benjamin Mkapa Hospital akidaka mpira mbele ya Restuta Boniface (kulia) na Salome Mika (WD) wa Ikulu katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo Ikulu walishinda kwa magoli 28-13.Nahodha wa timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) akikokota mpira pembeni ya beki Khalfan Mofu wa Wizara ya Nishati wakati wa mchezo wa michuano ya kombe la Mei Mosi iliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Nishati imeshinda bao 2-1.
*************************
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MABINGWA watetezi kwa michezo ya netiboli na soka timu za Ofisi ya Rais Ikulu na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) zimeendeleza ubabe kwa kushinda mechi zao katika michuano ya Kombe la Mei Mosi inayoendelea jijini hapa kwenye viwanja vya Jamhuri, Shell Complex, Kilimani na Mtelekezo Jijini Dodoma.
Katika netiboli timu ya Ikulu iliwafunga Benjamin Mkapa Hospital (BMH) kwa magoli 28-13. Washindi wenye kikosi chenye wachezaji mahiri na wenye uzoefu kubwa walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 13-6.
Nayo TANESCO alitoa kisago kikubwa kwa kuwafunga bila huruma Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa magoli 6-0, katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mtekelezo. Wachezaji walioipatia ushindi huo mnene na magoli waliyofunga yakiwa kwenye mabano ni Polycarp Ernest (3), Ibrahim Said (2) na Kurwa Mangara (1).
Katika michezo mingine timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) waliwachapa Wizara ya Kilimo kwa magoli 30-16. NCAA waliongoza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa magoli 17-7; huku timu ya Kongwa DC iliadabishwa kwa kufungwa na Hazina kwa kufungwa magoli 31-9. Hazina walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 19-2.
Nayo timu ya netiboli ya Uchukuzi SC waliwafunga Wizara ya Madini kwa magoli 43-9. Washindi waliongoza kipindi cha kwanza kwa magoli 22-5; nao Wizara ya Nishati waliwashinda Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa magoli 26-21. Hadi mapumziko Nishati waliongoza kwa magoli 12-10; huku timu ya Mzinga ikizinduka baada ya kupoteza mchezo mmoja na kuwafunga Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa magoli 33-16.
Halikadhalika, timu ya soka ya Uchukuzi SC waliwaliza ndugu zao Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kwa kuwafunga magoli 6-0. Magoli ya washindi yalifungwa na Idrisa Bahatisha (2), Lugano Mwasomola, Joseph Paul, Stephano Meta na Suleiman Kaitaba
Nayo Wizara ya Nishati iliwafunga Watoto wao Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kwa magoli 2-1, yaliyofungwa na Richard Richard na Charles Kitundu, wakati la TPDC lilifungwa na nahodha Dalushi Shija.
Nao TRA waliwafunga Wizara ya Afya kwa magoli 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Kilimani. Magoli ya TRA yalifungwa na Himran Ntabudyo na Maxmilian Maguncho; huku Wakala wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) walifungwa na NSSF magoli 4-2.
Michuano hii inayotarajiwa kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka tarehe 21 April, 2022