Mkuu wa Kituo cha Masomo ya Jinsia cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,Prof. John Jeckoniah akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari nje ya mkutano huo mara baada ya kuwasilisha matokeo ya utafiti wake
Meneja Mradi , Charles Leonard akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu malengo ya Warsha hiyo. |
Warsha ikiendelea. |
Na Calvin Gwabara, Morogoro
UTAFITI umeonesha kuwa Wanawake
hawajanufaika sana ikilinganishwa na Wauame katika kufikia na kutumia
rasialimali zinazopatikana kwenye misitu ya asili kama vile uchomaji na
biashara ya mkaa,mbao pamoja na rasiliamali zingine zinazopatikana kwenye
misitu hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kituo
cha Masomo ya Jinsia cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof.John Jeckoniah mara baada ya kuwasilisha
matokeo ya utafiti wake uliokuwa unaangalia maswala ya Jinsia na makundi
maalumu katika utumiaji,ufikiaji na wanavyonufaika na rasiliamali za
misitu.
“Katika utafiti wetu tumebaini kuwa
kuna changamoto kadhaa za kukosekana kwa uwiano wa kijinsia kwenye makundi
maalumu yanyoshiriki katika kutumia rasiliamali za misitu ya asili ambapo
imeonekana Wanawake hawanufaiki sana kama ilivyo Wanaume katika kufikia na
kunufaika nazo” Alibainisha Prof. Jeckoniah.
Amesema kuwa katika utafiti wao
walitakiwa kuangalia mikakati gani inayotumiwa na wadau mbalimbali wa maendeleo
ikiwa ni pamoja na Mtamdao wa kuhifadhi misitu ya asili Tanzania TFCG katika
kubuni mikakati mbalimbali za kuongeza ushriki wa makundi maalumu hasa
wanawake.
Prof. Jeckoniah amebainisha kuwa katika
wamebaini kazi kubwa imefanywa na mashirika hayo katika kuwajengea uwezo na
kuboresha Maisha na uchumi wa jamii kwenye vijiji mbalimbali vilivyofikiwa na
miradi ya TFCG na Mjumita lakini mara nyingi maswala ya kijinsia huangalia
zaidi Wanwake na kusahau Wanaume wakati nao wana mchango katika maamuzi na
maoni kwenye familia.
Kufuatia utafiti huo wanaona Wanaume
wakisahaulika kwenye mafunzo ya aina hiyo wakati wao ndio wanaotumika kutoa
mawazo na maoni pamoja na usimamizi wa wake yako chini ya Wanaume hivyo
wakisaulika wanweza kuwa kikwazo kwenye utekelezaji wake na kwenye maeneo
mbalimbali Wanawake wamelalamika kuwa wanaume ndio kikwazo katika mabadiliko
yao.
Akieleza malengo ya Warsha hiyo Meneja Mradi
wa CoFOREST ambao unatekelezwa na shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania
(TFCG) na Mtandao wa Jamii wa usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) bwana Charles
Leonard amesema lengo ni kuwashirikisha wadau na jamii matokeo ya tafiti
mbalimbali saba zinazohusu uhifadhi wa misitu zilizofanywa na watafiti kupitia
mradi wa CoFOREST.
“Lengo kuu ni kwanza wadau wapate uelewa
wa matokeo ya tafiti hizo, lakini lengo la pili ni wadau wapate nafasi ya
kuchangia na kutoa mapendekezo yao pamoja na kuchukua matokeo ya tafiti na
kwenda kuyaingiza kwenye utekelezaji wa shughuli wanazozifanya katika kuhifadhi
na kusimamia misitu hususani ya asili iliyo katika ardhi za vijiji nchini”
Alibainisha bwana Leonard.
Ametoa Rai kwa Serikali pamoja na wadau walio
kwenye sekta ya misitu hususani misitu ya asili kuwa kutokana na kutambua
umuhimu wa misitu hiyo kuna haja ya kuangalia ni namna gani misitu hiyo
inasimamiwa vizuri na kuzitumia rasilimali za misitu ya asili kwa kaisi abacho
kitapalelea uharibifu wa misitu unaotokea kwenye misitu iliyo kwenye ardhi za
vijiji ambayo haijahifadhiwa unakomeshwa.