Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akifungua kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwajuma Magwiza,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma’
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Tullo Masanja akitoa taarifa wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Amina Mfaki, akichangia jambo wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma.
Mtaalamu wa Mifumo kutoka USAID, Edwin Nyella,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini, kilichofanyika leo April 14,2022 jijini Dodoma.
……………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, imesema zinahitajika Sh.Bilioni 1.39 kugharamia uanzishaji wa mfumo wa jumuishi wa kielektroniki wa huduma za ustawi wa jamii nchini.
Hayo yameelezwa leo April 14,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo,Dkt.Doroth Gwajima wakati akifunga kikao cha wadau wa Maendeleo kinachojadili namna ya kuandaa mfumo Jumuishi wa huduma za ustawi wa jamii nchini.
Dkt.Gwajima amesema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kusanifu, kutengeneza hadidu za rejea, miundombinu, kuandaa wataalamu wa kutumia mfumo na kusambaza mfumo huo jumuishi nchi nzima.
“Ili kukamilisha mfumo huu pamoja na kuhakikisha unafanya kazi nchi nzima tunahitaji fedha za kitanzania 1.39 Bilioni” amesema Dkt. Gwajima
Hata hivyo Waziri Gwajima amewayataka mashirika ya maendeleo na wadau wote kuunga mkono juhudi za serikali moja kwa moja kwa kuelekeza rasilimali fedha na ujuzi katika eneo hili ili kuanzisha mfumo Jumuishi wa huduma za Ustawi wa Jamii ili kuboresha utoaji huduma.