Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Eliamani Sadoyeka akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa elimu kujadili rasimu ya “Tanzania Qualification Framework”uliofanyika leo Aprili 13,2022 Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Eliamani Sadoyeka akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa elimu kujadili rasimu ya “Tanzania Qualification Framework”uliofanyika leo Aprili 13,2022 Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Idara ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia) Dkt.Noel Mbonde akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa elimu kujadili rasimu ya “Tanzania Qualification Framework”uliofanyika leo Aprili 13,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wadau wa elimu nchini wakifuatilia ufunguzi wa kikao cha wadau wa elimu kujadili rasimu ya “Tanzania Qualification Framework” uliofanyika leo Aprili 13,2022 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Eliamani Sadoyeka akipata picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi za Elimu nchini wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa elimu kujadili rasimu ya “Tanzania Qualification Framework”uliofanyika leo Aprili 13,2022 Jijini Dar es Salaam.
****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
TQF nchini Tanzania inalenga kusawazisha na kuwianisha sifa na tuzo za kitaaluma za nchi kwa kutengeneza mfumo wa kuweka viwango, kuainisha maarifa yatakayotolewa, ili kutoa wataalamu wenye ujuzi unaotarajiwa/unaohitajika katika soko la ajira na utakaowawezesha wananchi kujiendeleza kielimu ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Ameyasema hayo leo Aprili 13,2022 Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Eliamani Sadoyeka, wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa elimu kujadili rasimu ya “Tanzania Qualification Framework”.
Amesema uandaaji wa Tanzania Qualifications Framework-TQF umefuata mfumo wa SADC Qualifications Framework (SACQF) lakini pia imezingatia matakwa ya soko la pamoja la Africa Mashariki.
Aidha amesema Mfumo huo umehusisha ngazi za elimu ya juu (High Education, elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET), elimu msingi (Basic Education) ambayo inahusisha elimu ya awali, msingi na sekondari na elimu ya watu wazima na mifumo isiyo rasmi.
Pamoja na hayo Prof.Sadoyeka amesema wakati wa mchakato wa kutengeneza NQF, Nchi zimekuwa zikiangalia muktadha wa kielimu, kijamii, kiuchumi na kisiasa pia.
“Miongozo mingi inayoandaliwa inafuata ajenda ya Elimu ya mwaka 2030 na SDG, lengo namba 4 ambalo linalenga kukuza elimu jumuishi na yenye usawa pamoja na fursa za kujifunza stadi za maisha”. Amesema Prof.Sadoyeka.