Adeladius Makwega –BUTIAMA
Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ametembelea banda la Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika nchini katika Viwanja vya Mwenge Butiama mkoani Mara huku akisema kuwa anatambua kuwa yeye ndiye aliyeizindua Programu hiyo mwaka 2011.
Akiongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Mheshimiwa Pauline Gekul (Mb), Waziri Mkuu Mstaafu Pinda pia amekuwa mgeni rasmi katika kuadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere Aprili 13, 1922 iliyotimia Aprili 13, 2022. Kijiji cha Mwitongo Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mara unakiona kitabu hiki cha kesi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya mwaka 1958 kilichoandikwa na Simon Ngh’waya.”
Huku Mkuu wa Mkoa wa Mara Ali Happi akiitikia kuwa ndiyo.
Akizunguka katika banda hilo mheshimiwa Pinda alikagua picha kadhaa za Wapigania Uhuru, huku Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika nchini ndugu Boniface Kadili akitoa maelezo hayo.
Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ilizinduliwa wakati wa Serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete ambapo katika tukio hilo mheshimiwa Kikwete alimtuma Mizengo Pinda Waziri Mkuu kwa wakati huo akiwa kumuwakilisha