Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Makame Mbalawa akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi alipotembelea banda laBenkihiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora.
Tanzania Commercial Bank TCB) imesema itaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo ili kuboresha uchumi wa Tanzania.
TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora mpaka Makutupora Mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya nne leo Mkoani Tabora
Moshingi amesema, Tanzania Commercial Bank ni benki kubwa nchini na wamejitoa na wameshiriki kwa hatua kubwa katika kuhakikisha shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanikisha mradi wa SGR Lot 4 kwa mafanikio makubwa.
“Tanzania commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC ni wenzetu hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio kwa mkoa wa Tabora,”amesema
“Kufanikiwa kwa mradi huu kutarahisha usafiri wa kutoka Tabora hadi Dar es Salaam kwa masaa sita, na treni ya mizigo kwa masaa kumi pia kutafungua fursa za kiuchumi kwa mikoa ya Tabora, Dodoma, Singida , Shinyanga hadi Mwanza,”amesema
Moshingi amesema, wananchi wa Tabora kwa sasa wataanza kukua kiuchumi, kwa kusafirisha mazao yao kwenda Dar es Salaam ambapo ndio soko kuu la biashara na usafiri utakuwani ni wa uhakika zaidi.