Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Imara Tech , Alfred Chengula akionyesha moja ya mashine wanayotengeza kwa ajili ya kusaidia wakulima .(Happy Lazaro)
***************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Kampuni ya utengenezaji wa mashine za kilimo ya Imara Tech iliyopo mjini hapa imebuni na kutengeneza mashine maalumu kwa ajili ya kupukuchua alizeti kwa lengo la kumkomboa mkulima pindi anapovuna mazao yake.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Alfred Chengula wakati akizungumza na waandishi wa habari na watafiti walipotembelea kampuni hiyo ikiwa ni mojawapo ya mafunzo kwa vitendo katika kujionea uzalishaji wa Zana mbalimbali ,mafunzo yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).
Alfred amesema kuwa, kampuni hiyo imekuwa ikibuni na kutengeneza mashine mbalimbali kwa ajili ya wakulima ikiwemo ya kukamulia alizeti ambayo imekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima wa zao hilo.
Amesema kuwa,mashine hiyo imeanzishwa kwa lengo kumsaidia mjasiriamali mdogo aliyepo kijijini ambapo imeweza kuwaongezea dhamani wakulima hao wanaozalisha mazao hayo ya alizeti kwa kiwango cha juu.
Chengula amesema,mashine hiyo ina uwezo wa kupukuchua gunia 25 kwa lisaa limoja ambapo kwa siku ina uwezo wa kupukuchua hadi magunia mia mbili.
“Tukiwapatia wakulima mashine hizo tumekuwa tukiwapata warrant ya mwaka mmoja ili kuondokana na changamoto ya uharibifu wa mashine hizo na wakulima wameweza kunufaika kwa kiasi kikubwa na kuweza kuongeza kilimo chenye tija”amesema.
Aidha amesema kuwa,wameweza pia kubuni mashine ya kuchakata na kubaraza chakula cha mifugo pamoja na mahindi na mashudu kwa ajili ya mifugo lengo likiwa ni kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji na kuweza kuongeza tija katika uzalishaji wao.
“kabla ya kutengeneza mashine hizo tunafanyaga utafiti wa kina ya mahitaji yaliyopo sokoni lengo likiwa ni kuondokana na changamoto ya ukosefu wa mashine hizo na kuweza kutengeneza kulingana na uhitaji na kwa kufanya hivyo tunawasaidia sana wakulima na wafugaji kupata mashine za kutosha na kuongeza kiwango cha uchumi”amesema Chengula.
Aidha alitoa wito kwa wakulima na wafugaji kujitokeza kwa wingi kuagiza mashine hizo bora na zenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi zinazotengenezwa kiwandani hapo ili kuweza kuboresha shughuli zao na kuwa za kisasa zaidi.