*****************
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, CGF Thobias Andengenye,
amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa hapa nchini.
Makamanda walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Zimamoto (SACF) Hamis Telemkeni, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha
Monitoring and Evaluation Makao Makuu Dodoma, anakwenda kuwa Kamanda
wa Zimamoto na Uokoaji (RFO) Mkoa wa Tanga.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto (SACF) Goodluck Urio,
aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (RFO) Mkoa wa Tanga,
anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro.
Aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (RFO) Mkoa wa Iringa,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto (SACF) Ambwene Mwakibete,
anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, nafasi
yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Isabela Mbwago.
Vilevile Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Jumbe Kondo, anakwenda kuwa
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji (RFO) Mkoa wa Njombe.
Pia aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro,
Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Gilbert Mvungi, amehamishiwa Makao
Makuu ya Zimamoto na Uokoaji Dodoma.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kutoa wito kwa Wananchi kuendelea
kutoa ushirikiano kwa Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mikoa na Wilaya
katika suala la Kinga na Tahadhari Dhidi ya majanga na maokozi.