Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na viongozi wa ghala la kuhifadhi kemikali ya Sulphur la kampuni ya African Inland Logistics ltd iliyopo mtaa wa Mamboleo kata ya Sandari Temeke Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kwenye ghala hilo leo Aprili 9,2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakitazama ghala la kuhifadhi kemikali ya Sulphur la kampuni ya African Inland Logistics ltd iliyopo mtaa wa Mamboleo kata ya Sandari Temeke Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kwenye ghala hilo leo Aprili 9,2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungmza na wananchi wanaoishi karibu na ghala la kuhifadhi kemikali ya Sulphur la kampuni ya African Inland Logistics ltd iliyopo mtaa wa Mamboleo kata ya Sandari Temeke Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kwenye ghala hilo leo Aprili 9,2022. Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikagua roli lililokuwa limebeba kemikali ya Sulphur la kampuni ya African Inland Logistics ltd iliyopo mtaa wa Mamboleo kata ya Sandari Temeke Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kwenye eneo hilo leo Aprili 9,2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikagua roli lililokuwa limebeba kemikali ya Sulphur la kampuni ya African Inland Logistics ltd iliyopo mtaa wa Mamboleo kata ya Sandari Temeke Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kwenye eneo hilo leo Aprili 9,2022.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiumwagikaji wa kemikali ya Sulphur ya kampuni ya African Inland Logistics ltd iliyopo mtaa wa Mamboleo kata ya Sandari Temeke Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kwenye eneo hilo leo Aprili 9,2022. Kemikali ya Sulphur ikiwa kwenye ghala la uhifadhi kemikali hiyo.
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa siku saba kufungwa kwa ghala la kuhifadhi kemikali ya Sulphur ili waone ni namna gani wanaweza kudhibiti kemikali hiyo isiweze kuwadhuru wnanchi waliopo karibu na ghala hilo.
Ametoa agizo hilo leo Aprili 9,2022 mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mtaa wa Mamboleo kata ya Sandari Temeke Jijini Dar es Salaam na kusikiliza kero kwa wananchi kuhusu ghala hilo.
“Nasimamisha shughuli zote katika ghala hili kwa muda wa siku saba, lakini mkiweka miundombinu inayolinda mazingira kabla ya muda huo shughuli zenu zinataendelea. Wananchi wanaangaika, wanateseka nanyi hamjari hilo sasa kama hamtajirekkebisha kwa muda huo shughuli zote zitasitishwa kabisa”. Amesema Waziri Jafo.
Waziri Jafo amesema kuna umuhimu wa kampuni hiyo kufanya tathimini ya mazingira ili kuhakikisha kwamba katika shughuli ambayo wanaifanya haiwezi kuathiri mazingira kwa njia yoyote ile.
Kwa upande wake Meneja wa NEMC kanda ya Kusini Mashariki Bw.Hamad Taimuru amesema kiwanda hicho kinatakiwa kutumia mifuko maalumu ya kufungashia kemikali hiyo ili pale Maroli yakiwa yanabeba kemikali ya sulphur isiweze kumwagika na kuweza kuleta madhara kwa wananchi.
Hata hivyo kwa upande wa wananchi kwa ujumla wamemshukuru Waziri Jafo kwa kuweza kutembelea eneo hilo hivyo matumaini yao kushuhudia changamoto hizo wanazozipata zitashughulikiwa na kuondokana na kero hiyo.